TANGAZO
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MJI WA MASASI.
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI.
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI
ANAWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA WOTE KUWA NA LESENI HAI ZA BIASHARA.
LESENI ZA BIASHARA KWA MWAKA MPYA WA SERIKALI 2016/2017
ZIMEANZA KUTOLEWA TANGU TAREHE 1/07/2016 NA KWAMBA WALE WOTE WATAKAOSHINDWA
KULIPA NDANI YA SIKU 21 WATATOZWA FAINI.
KUMBUKA KUENDESHA BIASHARA BILA KUWA NA LESENI HAI
NI KINYUME NA SHERIA YA LESENI ZA BIASHARA NA.25 YA MWAKA 1972 NA.3 (1, 2 &
3).
MFANYABIASHARA YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUFANYA
BIASHARA KINYUME NA SHERIA HII ATACHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA KAMA
ILIVYOAINISHWA KATIKA KIFUNGU NA.10 (1) & (2).
MWISHO WAFANYABIASHARA WOTE WANASISITIZWA KUFUATA
MASHARTI YA LESENI,IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA LESENI ZAO SEHEMU ZA WAZI KATIKA
MAENEO YAO YA BIASHARA KWANI KUTOFANYA HIVYO NI KWENDA KINYUME NA MATAKWA YA
SHERIA YA LESENI KIFUNGU NA. 14 (1).
Clarence Chilumba,
Ofisa Habari Halmashauri ya Mji wa Masasi
Julai 16,2016.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD