TANGAZO
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizindua duka la dawa la MSD kwenye hospitali ya Wilaya ya Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016.Kushoto kwake ni mkewe Mary na watano kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa na kushoto kwa Waziri Mkuu ni Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amefungua duka la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) katika Hospitali ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi ambalo litakuwa na uwezo wa kuhudumia hospitali 524 katika mikoa ya Lindi, Mtwara na wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma.
Akizindua duka hilo leo (Jumamosi, Julai 16, 2016) Waziri Mkuu amesema duka hilo litaendelea kuboresha huduma za upatikanaji wa dawa kwa gharama nafuu katika hospitali, vituo vya afya na zahanati katika wilaya ya Ruangwa pamoja na mikoa na wilaya za jirani.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa Majakipokea miguu miwili ya bandia kabla ya kuzindua duka la dawa la MSD lililokwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa Julai 16, 2016. Miguu hiyo imetengeezwa na kutolewa msaada Kampuni ya Kamal Steel kwa wananchi wawili wa wilaya ya Ruangwa. Watatu kushoto ni Mke wa Waziri Mkuu, Mary Majliwa na wapili kushoto ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa wa Lindi, Ali Mtopa.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza baada ya kuzindua duka la dawa la MSD kwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa akiwa katika ziara ya jimbo lake la uchaguzi Julai 16, 2016.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizi ndua duka la dawa la MSD baada ya kulizindua kwenye hospitali ya wilaya ya Ruangwa Julai 16, 2016. Kulia kwake ni mkewe Mary.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD