TANGAZO
OFISI YA RAIS
TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MJI WA MASASI
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ANAWATANGAZIA WAFANYABIASHARA WOTE WALIOPANGA BIASHARA ZAO PEMBEZONI MWA BARABARA KUU YA MTWARA-MASASI ZIKIWEMO SARUJI,CHUMVI,NGUO,SOFA NA NYINGINEZO NYINGI KUWA WANATAKIWA KUONDOA BIASHARA HIZO MARA MOJA KWANI HUO NI MOJA YA UCHAFU.
KIKOSI KAZI KIKIONGOZWA NA OFISI YA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI KIMEPANGA KUFANYA OPERESHENI MAALUMU ITAKAYOANZA KESHO JUMATANO JULAI 27,2016 YA KUONDOA VIBANDA VIDOGO VIDOGO VYA BIASHARA VILIVYOJENGWA PEMBEZONI MWA BARABARA KUU BILA YA KUPATA KIBALI KUTOKA KWA MAMLAKA HUSIKA LENGO LIKIWA NI KUIFANYA MASASI IWE SAFI.
OPERESHENI HII NI MAALUMU AMBAYO INALENGA KUWAONDOA WAFANYABIASHARA WOTE WANAOENDESHA BIASHARA ZAO NDANI YA MJI WA MASASI PASIPO KUFUATA UTARATIBU MAALUMU UNAOTOLEWA NA WATAALAMU WA MIPANGO MIJI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI.
AIDHA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ANAWAKUMBUSHA WANANCHI WOTE WA MJI WA MASASI KUWA WIKI YA USAFI WA MAZINGIRA IMEANZA RASMI JULAI 25 NA KILELE KITAKUWA JULAI 30 AMBAPO KIMKOA KITAFANYIKA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI KUANZIA SAA 12:00 ASUBUHI HADI SAA 4:00 ASUBUHI.
ENEO AMBALO TUNATARAJIA KUKUTANA SIKU YA KILELE CHA USAFI WA MAZINGIRA JULAI 30,2016 NI ENEO LA MAKUTANO YA BARABARA KUU YA MTWARA,TUNDURU,MASASI AMBAPO MGENI RASMI MKUU WA MKOA WA MTWARA ATAZINDUA ZOEZI HILO NA BAADAE WANANCHI WATAENDELEA NA USAFI WA MAZINGIRA KATIKA MAENEO YAO.
Limetolewa na,
Kitengo cha Habari na Uhusiano,
Halmashauri ya mji,
MASASI.
Julai 26,2016.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD