TANGAZO
MKUU
WA MKOA WA MTWARA KUWAONGOZA WANA MASASI SIKU YA USAFI JULAI 30, 2016.
Siku ya usafi wa mazingira hufanyika kila Jumamosi ya
mwisho wa mwezi kote nchini ambapo kwa upande wa Halmashauri ya mji wa Masasi usafi
utafanyika kimkoa siku ya tarehe 30/7/2016 kuanzia saa 12:00 asubuhi hadi saa
10:00 asubuhi.
Miongoni mwa viongozi wanaotarajiwa kuongoza zoezi hilo
ni mkuu wa mkoa wa Mtwara atakayeambatana na wakuu wa wilaya za mkoa wa Mtwara
pamoja na wakurugenzi wa wilaya,manispaa na miji mkoani humo.
Shughuli kubwa itakuwa ni kufanya usafi wa mazingira
kwenye maeneo mbalimbali ya Mji kwa kushirikisha timu ya Mkuu wa Mkoa wa
Mtwara, viongozi mbalimbali ngazi za Wilaya, Halmashauri, kata, vijiji na mitaa
ikiwa ni pamoja na wananchi wote wa Masasi.
Katika siku hiyo
shughuli zote za kiofisi, kijamii na kibiashara zitasimama kipindi chote cha
zoezi hilo ili kuruhusu wananchi wote kushiriki kikamilifu kufanya usafi wa
mazingira kwenye maeneo yao.
Shughuli za usafi wa
mazingira zitaanza rasmi tarehe 25/7/2016 na zitaendelea mpaka siku ya kilele yaani
tarehe 30/7/2016 ambapo wananchi wote watafanya usafi kwenye maeneo yao ya
makazi na biashara.
Kwa upande wa Halmashauri
ya Mji wa Masasi tayari maandalizi yameshaanza ikiwa ni pamoja na kufanya
uhamasishaji jamii kwa njia ya matangazo ya gari, Radio, Ujumbe mfupi wa simu
za mkononi, matangazo ya mabango ya vitambaa yatakayowekwa kwenye njia kuu, kutoa
matangazo kwenye nyumba za ibada pamoja na kuongea na viongozi mbalimbali wa
vyama vya siasa.
Baadhi ya Viongozi wa vyama
vya siasa akiwemo Mheshimiwa Mbunge wa
jimbo la Masasi na waheshimiwa madiwani wote wa jimbo la Masasi watashirikishwa
kikamlifu katika kufanikisha zoezi hili la usafi wa mji wa Masasi lakini pia watu maarufu kwenye jamii na maafisa watendaji
wa kata na mitaa wote watashiriki kuhamasisha jamii.
Ewe Mkazi wa mji wa Masasi
jitokeze kufanya usafi pamoja na mkuu wa mkoa wa Mtwara siku ya tarehe
30/07/2016 kuanzia saa 12:00 Asubuhi hadi saa 4:00 Asubuhi.
kauli mbiu: “Ona
aibu kuishi na uchafu, ifanye Masasi iwe safi”
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD