TANGAZO
Vyumba Tisa vya madarasa vimeteketea katika shule ya sekondari ya Lindi, kufuatia kuzuka kwa moto mkubwa ulioanza kuwaka majira ya saa Saba za usiku kutokana na hitilafu kwenye mfumo wa umeme.
Kamanda
wa polisi wa mkoa wa Lindi Renata Mzinga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo
na kusema kuwa, mbali na vyumba hivyo, athari zingine zilizotokana na moto huo
ni kuteketeza matundu 26 ya vyoo, ofisi 4 za walimu pamoja na vyumba viwili vya
maabara za Kemia na Fizikia.
“Ulianzia
kwenye ‘Main switch’..chumba ambacho kina ‘Main Switch’ kwa mujibu wa mtoa
taarifa za awali ambaye ni mwalimu wa shule hiyo na kwa sababu pale shuleni hakuna
namna ya kuingiza zima moto
Na
Kusema……
Miundombinu
ilizuia kuingiza gari la zima moto kwa hiyo wananchi wakawa wanajitahidi kuuzima
kwa kuchota maji hiyo ikapelekea moto kusambaa..”alisema Kamanda.
Aidha,
alisema hakuna madhara mengine yoyote yaliyojitokeza dhidi ya binadamu na
kwamba bado wanafunzi walikuwa hawajaanza kuwasili shuleni hapo kutoka makwao
walikokuwa kwa likizo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD