TANGAZO
Ofisa Biashara wa Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara Masoud Mwinjuma (kulia) akimwamuru kufunga Banda la Biashara yake mmoja wa wafanyabiashara ya Salon katika eneo la Nyasa Magengeni kwa kosa la kuendesha Biashara hiyo pasipo kuwa na Kibali au Leseni.
TAARIFA KWA UMMA KUPITIA VYOMBO VYA HABARI.
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI
ANAWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA WOTE KUWA NA LESENI HAI ZA BIASHARA.
LESENI ZA BIASHARA KWA MWAKA MPYA WA SERIKALI
2016/2017 ZITAANZA KUTOLEWA KESHO TAREHE 1/07/2017 NA KWAMBA WALE WOTE
WATAKAOSHINDWA KULIPA NDANI YA SIKU 21 WATATOZWA FAINI.
KUMBUKA KUENDESHA BIASHARA BILA KUWA NA LESENI HAI
NI KINYUME NA SHERIA YA LESENI ZA BIASHARA NA.25 YA MWAKA 1972 NA.3 (1, 2 &
3).
MFANYABIASHARA YEYOTE ATAKAYEBAINIKA KUFANYA
BIASHARA KINYUME NA SHERIA HII ATACHUKULIWA HATUA KALI ZA KISHERIA KAMA
ILIVYOAINISHWA KATIKA KIFUNGU NA.10 (1) & (2).
MWISHO WAFANYABIASHARA WOTE WANASISITIZWA KUFUATA
MASHARTI YA LESENI,IKIWA NI PAMOJA NA KUWEKA LESENI ZAO SEHEMU ZA WAZI KATIKA
MAENEO YAO YA BIASHARA KWANI KUTOFANYA HIVYO NI KWENDA KINYUME NA MATAKWA YA
SHERIA YA LESENI KIFUNGU NA. 14 (1).
Clarence Chilumba,
Ofisa Habari Halmashauri ya Mji wa Masasi
30/06/2016.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD