TANGAZO
Na Bashiru Kauchumbe,Ruangwa.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni mbunge wa
jimbo la Ruangwa mkoani Lindi Mhe Kassimu Majaliwa kesho anatarajia kuanza ziara ya siku tatu Wilayani Ruangwa.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na mkuu wa Wilaya ya Ruangwa
Mariamu Mtima alisema ziara hiyo ya
kikazi itaanza kesho jumapili ya April 10,2016.
Katika ziara hiyo Majaliwa
atapokelewa na Uongozi wa Wilaya ya Ruangwa katika kijiji cha Likunja majira ya
saa 9.30 alasili ambapo atapata fursa ya kuongea na wananchi wa kijiji hicho na kwamba Pia siku
hiyo hiyo ataongea na wananchi wa kijiji cha Kitandi majira ya saa 11:00 za
jioni.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya alisema Siku ya pili ya ziara yake Mh: Majaliwa ataweka
jiwe la msingi jengo la Bohari ndogo ya kuhifadhia Madawa katika Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa
pamoja na uzinduzi wa chumba cha kutunzia watoto waliozaliwa wakiwa njiti.
Aidha atatembelea katika Hospitali
ya Wilaya ya Ruangwa kwa lengo la kuona
wagonjwa pamoja na kuangalia mazingira ya utendaji kazi katika Hospitali
hiyo,Majaliwa atakamilisha ziara yake siku ya pili kwa kutembelea Soko kuu la
Wilayani humo na mwisho ataongea na watumishi wa Wilaya ya Ruangwa.
Siku ya tatu ya ziara yake waziri mkuu huyo atapata nafasi ya kuongea na
wanawake wa wilaya ya Ruangwa katika ukumbi wa chama cha walimu wilayani
humo.
Katika ziara hiyo waziri mkuu Mh: Kasimu Majaliwa atafanya mikutano ya
hadhara katika vijiji vya Nkowe,Luchelegwa ,Chinongwe na Nanganga na hatimaye
kuondoka kuelekea Mjini Lindi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD