TANGAZO
Na
Bashiru Kauchumbe,Ruangwa.
MKAZI
wa kijiji cha Dodoma wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi Alapha Matingo (40) amepoteza baadhi ya viungo vyake ikiwemo
macho yake baada ya kufanyiwa vitendo vya kikatili ikiwemo kipigo kutoka kwa
wanaume wawili tofauti.
Akisimulia
mkasa huo Matingo alisema mwaka 2007 akiwa anaishi na mume wake aliyejulikana kwa jina la Kiweru Abdallah Mkazi
wa Kilimahewa wilayani alipigwa vibaya na mume wake baada ya kuhoji tabia ya
mume huyo kurudi usiku wa manane akiwa amelewa.
Alisema kutokana na kipigo hicho jicho lake moja la upande wa
kushoto lilipata majeraha makubwa na hatimaye kupasuka na alikimbizwa katika
hosiptali ya rufaa ya Ndanda wilayani Masasi ambako hata hivyo jicho hilo
halikuweza kuona tena na kuwekewa jicho la bandia.
“Ilikuwa ni siku ambayo siwezi kuisahau katika maisha yangu…mume
wangu alirudi nyumbani usiku majira ya saa 5:00 akiwa amelewa na bila kuuliza
chochote alianza kunipiga mwili mzima na akafanikiwa kupasua jicho langu la
kushoto nilikimbizwa hospitali lakini madaktari hawakufanikiwa kutibu na
hatimaye waliniwekea jicho la bandia”alisema Matingo.
Alisema baada ya tukio hilo mume wake alikamatwa na jeshi la polisi
wilayani Ruangwa na kufikishwa mahakamani ambapo alifungwa kifungo cha miaka
mitatu jela.
Kwa mujibu wa Alapha Matingo alisema mwanzoni mwa
mwaka 2012, aliolewa tena na mume mwingine aliyejulikana kwa jina la Ndoje
Athumani ambapo Desemba mwaka huo alikumbwa na mkasa mwingine wa kupigwa vibaya
kwenye jicho lake la pili lililopasuka papo hapo.
Alisema kipigo hiko kilimsababishia mauimvu makali na hatimaye
jicho lake kuondolewa na kubaki mlemavu wa macho hadi sasa mazingira
yaliyomsababishia kuishi katika mazingira magumu kutokana na ulemavu huo wa
macho.
Alisema
katika hatua isiyo kuwa ya kawaida mume wake huyo hakuchukuliwa hatua zozote za
kisheria na ameendelea kufurahia maisha huku yeye akiwa anaishi kwa shida kwa
kutokuona kwake huku jukumu la kumtunza mume wake huyo likibaki kuwa lake.
Kwa
upande wake Ndoje Athumani ambaye hadi leo hii anaishi na mke wake huyo mlemavu
wa macho alipotakiwa kutoa maelezo alikiri kutenda kosa hilo huku akijutia
maamuzi hayo ambapo alisema kilichosababisha kufanya maamuzi hayo ni unywaji
wake wa pombe kupita kiasi huku akitoa ahadi ya kutomuacha mke huyo hadi mwisho wa maisha yake.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD