TANGAZO
Na Boppe Kyungu,Mkuranga.
Mratibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya jipeni Moyo Wanawake Community Organisation (JIMOWACO)
Israel Musyangi amewataka wananchi wa wilaya ya
Mkuranga mkoani Pwani kuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara
kwa lengo la kubaini afya zao.
Aliyasema hayo jana wilayani humo wakati wa kampeni ya uhamasishaji na
upimaji wa virusi vya Ukimwi na Malaria kwa wananchi wa kata za Bupu na
Mwarusembe ambapo alisema uhamasishaji huo ulianza Julai 2015 na unatarajia
kukamilika Julai 2016.
Alisema hadi sasa zoezi hilo la uhamasishaji limefanyika katika kata 20 za wilaya ya Mkuranga na kwamba
kwa sasa wanatarajia kukamilisha katika kata tano zilizobaki baada ya kupata
fedha kutoka kwa wafadhili wa mradi huo.
Alisema katika kata ya Mwarusembe waliojitokeza kupima Malaria ni 50
ambapo kati yao waliogundulika kuwa na malaria ni 11 ambapo kwa upande wa kata
ya Bupu wilayani humo waliojitojeza kupima malaria ni 50 huku waliokutwa na
virusi vya ugonjwa huo ni 16 pekee.
“Kauli mbiu ya zoezi hili ni Si
Kila homa ni Malaria… ambapo ili kubaini unaumwa nini ni vyema sasa wananchi
muwe na utamaduni wa kupima afya badala ya kufanya vitu kwa mazoea au kunywa
dawa za malaria bila hata kupima” alisema Musyangi.
Aidha kwa upande wa upimaji wa Virusi vya Ukimwi kwa kata ya Mwarusembe waliojitokea kupima ni wananchi
48 ambapo waliogundulika kuwa na maambukizi ya
Virusi vya Ukimwi ni wawili na kwa Kata ya Bupu waliopima ni 29 kati yao
wanawake ni 13 na wanaume 19 na kwamba
hakuna mtu aliyekutwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.
Kwa mujibu wa Mratibu huyo alisema mradi wa Tanzania Communication
Development Center ulianza mwaka
2015 na kwamba kwa sasa kinachofanyika
ni muendelezo wa mradi huo huku kukiwa na ongezeko la upimaji wa Virusi vya
Ukimwi ,afya ya mama na mtoto, pamoja na kifua kikuu.
Issa Athumani (17) mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari
Mamdi kongo kata ya Bupu ambaye baada ya vipimo alikutwa na malaria alisema
katika kipindi cha miezi mitano iliyopita alikuwa anapata maumivu makali ya kichwa huku akishindwa kutambua tatizo hadi
alipopima wakati wa kampeni hiyo na kugundulika na tatizo la Malaria.
Kwa upande wake muelimishaji jamii wa kata ya Mwarusembe Mohammed
Kisilwa alisema ni vyema wananchi kila wanapohisi kuwa na dalili za ugonjwa wa Malaria ni vyema wakaenda
hospitali kwa lengo la kujua matatizo mbalimbali
yanayowakabili kwenye miili yao.
Jipeni Moyo Wanawake Community Organisation (JIMOWACO) ni taasisi isiyo
ya kiserikali iliyoanzishwa mwaka 2002,
yenye makao makuu yake Kisarawe Mkoani Pwani, ikiwa na lengo la kusaidia akinamama
hususani wenye maambukizi ya Virusi vya
Ukimwi waweze kujikwamua kiuchumi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD