Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

JE,WEWE NI MIONGONI MWA WATU WALIOLIPIA VIWANJA VYA STENDI MPYA MASASI? HII HAPA INAKUHUSU

TANGAZO

TANGAZO KWA WALIOLIPIA VIWANJA VYA STENDI MPYA YA MABASI (MIESI) MJINI MASASI.
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE WA MJI WA MASASI WALIOLIPIA VIWANJA KATIKA ENEO LA MIESI LITAKALOJENGWA STENDI MPYA YA MABASI KUWA WANATAKIWA KUJA KUHAKIKI MAJINA YAO.

ZOEZI HILO LA UHAKIKI WA MAJINA YA WANANCHI WALIOLIPIA VIWANJA HIVYO LITAANZA SIKU YA JUMANNE YA TAREHE 29/03/2016 HADI TAREHE 01/04/2016 KATIKA OFISI YA ARDHI HALMASHAURI YA MJI WA MASASI KUANZIA SAA 3:00 ASUBUHI HADI SAA 9:30 JIONI.

ORODHA YA MAJINA YA WANANCHI WOTE WALIOLIPIA VIWANJA VYA HUKO MIESI ITABANDIKWA KWENYE MBAO ZA MTANGAZO ZILIZOPO KATIKA OFISI YA IDARA YA ARDHI HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ILI KILA MUHUSIKA AONE JINA NA NAMBA YAKE YA KIWANJA ALICHOLIPIA.

AIDHA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI ANAWATAARIFU WANANCHI HAO KUWA BAADA YA ZOEZI HILO LA UHAKIKI WA MAJINA KUKAMILIKA KUTAKUWA NA KIKAO CHA PAMOJA KATI YA WANANCHI HAO PAMOJA NA WAKUU WA IDARA WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI KITAKACHOFANYIKA SIKU YA JUMAMOSI YA TAREHE 02/04/2016 KATIKA UKUMBI WA MIKUTANO WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI KUANZIA SAA 3:00 ASUBUHI.

KATIKA KUFANIKISHA ZOEZI HILI MUHIMU KWA MAENDELEO YA MJI WA MASASI WANANCHI WOTE MLIOLIPIA VIWANJA MNAPASWA KUSHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA HATUA ZOTE MUHIMU ZA MCHAKATO HUU IKIWEMO UHAKIKI WA MAJINA PAMOJA NA KUSHIRIKI SIKU YA KIKAO CHA PAMOJA NA UONGOZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI.

LENGO LA MCHAKATO HUO NI KATIKA KUHAKIKISHA KWAMBA KILA MWANANCHI ALIYELIPIA VIWANJA HIVYO ANASHIRIKI KIKAMILIFU KATIKA HATUA ZOTE KABLA YA ZOEZI RASMI LA UJENZI WA STENDI HIYO MPYA NA YA KISASA HALIJAANZA MAPEMA MWEZI APRIL 2016.

“EWE MWANANCHI KUMBUKA USHIRIKI WAKO KATIKA ZOEZI HILI NI CHACHU YA MAENDELEO KATIKA MJI WA MASASI”.

KWA MAELEZO YA KINA NA UFAFANUZI ZAIDI TEMBELEA www.masasitc.go.tz Au sikiliza Vipindi vya Redio vya Fadhila Fm) 95.0) Mjini Masasi pamoja na Matangazo ya Barabarani (PA).

WOTE MNAKARIBISHWA!!!!!!

Clarence Antony Chilumba,
Ofisa Habari na Uhusiano,
Halmashauri ya Mji wa Masasi.
24/03/2016.



TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top