TANGAZO
Selemani Jafo,Naibu waziri Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Picha ya Maktaba).
Naibu Waziri Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mheshimiwa Selemani Jafo amewaagiza
Wakurugenzi wa Halmashauri na Manispaa nchini kuandaa utaratibu wa kuwapeleka
Wenyeviti na Mameya kupata mafunzo ya uongozi katika Chuo cha Serikali za Mitaa
Hombolo kilichopo mkoani Dodoma.
Akizungumza mara baada ya
ziara yake ya kukitembelea chuo hicho, mhe Jafo alisema kwa kuwa uchaguzi mkuu
umepita na Madiwani wameshachaguliwa wanatakiwa wapewe mafunzo maalumu ya muda
mfupi juu ya namna ya kusimamia na kuendesha halmashauri zao.
“Ninawaagiza Wakurugenzi
wote wa Halmashauri kuwasiliana na Ofisi ya Rais Tamisemi ili kujua namna ya
kuwawezesha nauli Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Halmashauri na Mameya na
Manaibu Meya kuja Chuoni Hombolo kwa siku tatu au tano kupata mafunzo juu ya
uendeshaji wa Mamlaka za Serikali za Mitaa”.alisema.
Naibu Waziri huyo alisema
ni vyema mafunzo hayo yakaanza na Wenyeviti wa Halmashauri, Makamu Wenyeviti,
Mameya na Manaibu Meya ili kuwajengea uwezo Viongozi hao wa mamlaka za Serikali
za Mitaa na kwamba ikiwa katika halmashauri 185 Madiwani wake wakiwezeshwa
watakuwa na uelewa mpana wa masuala yanayohusu mikataba na malipo katika
halmashauri zao.
Alisisitiza kuwa gharama
wanazotakiwa kuwezeshwa katika halmashauri zao ni nauli tu kwani na kwamba
Wakurugenzi hawatakiwi kuwalipa posho Wenyeviti hao wa halmashauri kwa kuwa
kila kitu kinachohusu mafunzo hayo kitasimamiwa na Ofisi ya Rais Tamisemi kwa
kushirikiana na Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo.
Aidha alisema baada ya
mafunzo hayo Madiwani wengine watapata mafunzo hayo katika maeneo yao au
kupitia Kanda zao kulingana na utaratibu wa Chuo kitakavyopanga.
Kwa upande wake Mkuu wa
Chuo hicho Dkt. Emanuel Gibai alisema Uongozi wa Chuo upo tayari kutoa mafunzo
hayo kwa kuwa Wana watumishi wanaolipwa na Serikali kwa ajili ya mafunzo
yanayohusu Serikali za Mitaa.
Alisema Chuo kina mabweni
na madarasa ya kutosha kuwapokewa Madiwani hao wa Halmashauri watakaokuja
wakati huu ili kuwajengea uwezo wa kuyahudumia maeneo yao.
Alisema kwa kipindi hiki
ambapo Wanafunzi wamefunga chuo wanatarajia mafunzo hayo ya Wenyeviti na Makamu
wenyeviti pamoja na Mameya na Manaibu meya yafanyike kati ya tarehe 10 na 20
januari ya mwaka 2016 katika Chuo hicho
Alisema Chuo kina
wataalamu waliobobea katika uongozi wa Serikali za Mitaa na wapo tayari
kuwafundisha madiwani wote pamoja na Viongozi wengine wa Serikali kwa utaratibu
utakaopangwa na Wizara.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD