TANGAZO
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Mathew Kagoro
TANGAZO
MKURUGENZI
WA MJI WA MASASI ANAWATANGAZIA WANANCHI WOTE KUFANYA USAFI WA MAZINGIRA KUZUNGUKA
NYUMBA ZENU, MAENEO YA BIASHARA ZENU, OFISI NA KUSAFISHA MIFEREJI YA BARABARA
ZILIZOPITA MBELE YA NYUMBA ZENU.
PIA
SIKU YA JUMAMOSI TAREHE 05/12 NA 09/12 NI SIKU ZA KUFANYA USAFI KWA PAMOJA
KATIKA MAENEO YA KAUMU, MKUTI SOKONI NA MKOMAINDO HOSPITALI.
HIVYO
WANANCHI WOTE MNAOMBWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUFANYA USAFI KATIKA MAENEO HAYO
KUANZIA SAA 12:00 HADI SAA 3:00 ASUBUHI AMBAPO BIASHARA ZOTE ZITAFUNGWA KURUHUSU
WANANCHI WOTE KUSHIRIKI KUFANYA USAFI.
NI
MARUFUKU KUWEKA TAKATAKA MBELE YA NYUMBA, KANDOKANDO YA BARABARA, KUCHOMA TAKA,
KUTUPA AU KULIMA MAZAO YANAYOZIDI KIMO CHA FUTI 3 KAMA VILE MAHINDI, MBAAZI NA
MTAMA KATIKA MAKAZI YA WATU.
AIDHA
UKAGUZI WA NYUMBA KWA NYUMBA UTAFANYIKA KILA SIKU KUANZIA SASA, WALE
WATAKAOKUTWA MAZINGIRA YAO NI MACHAFU WATATOZWA FAINI YA TSHS. 50,000/=
"USAFI
NI USTAARABU, UNAANZA NA SISI"
LIMETOLEWA
NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI.
FORTUNATUS MATHEW KAGORO.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD