TANGAZO
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji mstaafu Damian Lubuva.
MWENYEKITI wa Tume
ya Uchaguzi (NEC) Jaji Mstaafu Damian Lubuva, amewataka makamanda wa
polisi wa Mikoa ya Tanzania bara pamoja na Zanzibar na mawakala wa uchaguzi
kuhakikisha wanatenda haki ili uchaguzi wa mwaka huu uwe wa uhuru,
amani na haki.
Akizungumza jijini
Dar es Salaam jana, Jaji Lubuva, alisema kosa dogo linaweza kuleta uvunjifu wa
amani katika uchaguzi huo hivyo tume imeamua kushirikiana na Jeshi la Polisi
ili kuwapata uelewa kuwezesha utekelezaji wa majukumu yao katika uchaguzi
mkuu.
Alisema katika
chaguzi zilizo pita Tume ilikua ikifanya mikutano tofauti ambapo ilikuwa
inakutana na watendaji wa uchaguzi peke yake na makamanda wa polisi peke yake,
hivyo mkutano wa mwaka huu ni tofauti na mikutano iliyopita.
Jaji Lubuva alisema
ili uchaguzi uwe wa huru na haki ni lazima uendeshwe katika hali ya utulivu na
amani na hali ya usalama ili kuwezesha wapiga kura kutumia haki yao ya
kikatiba kwa kwenda vituoni kupiga kura bila ya kuwa na hofu.
"Jeshi la
polisi lina jukumu la kuhakikisha hali ya usalama na amani katika kipindi cha
uchaguzi ndiyo maana Tume imeamua kushirikiana Jeshi la Polisi kulinda
amani," alisema Jaji Libuva.
Alisema wadau hao
wote wana jukumu la kusimamia zoezi hilo zima ili liweze kumalizika kwa
usalama, kwani kosa moja linaweza kusababisha uvunjifu wa amani katika maeneo
mbalimbali ya nchi.
"Ni muhimu
kufanya kazi zenu kwa weledi mkubwa,uadilifu na kwa kufata sheria,kanuni na
taratibu za uendeshaji uchaguzi kama ilivyoelekeza na Tume ya Uchaguzi,"
alisema Jaji Lubuva.
Jaji Libuva alisema
katika chaguzi zilizopita kulikuwepo na changamoto ya makundi ya vijana
wanaohisiwa kuwa wafuasi wa vyama vya siasa kwa kuwatishia wapigakura hususani
akinamama ili wasiende kupiga kura,ambapo hilo linawasababishia watu kukosa haki
ya msingi ya kupiga kura.
Naye Inspekta wa
Polisi (IGP) Ernest Mangu, alisema watahakikisha uchaguzi unaenda kwa amani
bila kuleta madhara kwa wapiga kura.Alisema hawataruhusu mpiga kura kubaki
katika vituo vya kupigia kura kwani mawakala wa kila chama wana jukumu la
kulinda kura za vyama vyao.
Aliongeza kuwa kila
mdau analo jukumu la kufanya kazi na kuhakikisha kuwa uchaguzi unafanyika
katika mazingira ya amani na utulivu.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD