TANGAZO
KATIBU tawala wa wilaya ya Masasi Danford Peter (kushoto) akimpongeza meneja mauzo wa kampuni ya Vodacom wilaya ya Masasi Angetile Martin (kulia) mara baada ya kukamilika kwa zoezi la uzinduzi wa duka la kampuni hiyo mjini Masasi hii leo.
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
KAMPUNI ya simu za mkononi
ya Vodacom imezindua rasmi duka kubwa na
la kisasa la bidhaa za kampuni hiyo lengo likiwa ni kusogeza huduma kwa
wananchi wa wilaya ya Masasi ili kuendana na kasi ya maendeleo ya sayansi na
teknolojia.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi wa duka hilo katibu tawala wa wilaya ya Masasi Danford Peter aliwataka
wafanyakazi wa kampuni hiyo tawi la Masasi kutoa huduma zao bila upendeleo
sambamba na lugha nzuri kwa wateja wao ili waweze kupata wateja wa kutosha.
Alisema serikali inatambua
mchango wa kampuni hiyo ya simu za mkononi ya Vodacom katika kuinua kipato cha
wananchi wa Tanzania kupitia baadhi ya huduma zake ikiwa ni pamoja na huduma ya
M-Pawa inayomwezesha mteja wa Vodacom kuweka akiba na kupata mkopo usio na
vigezo vyovyote.
Alisema kampuni ya Vodacom
ni miongoni mwa kampuni kubwa ya
mawasiliano nchini na kwamba kuwepo kwa kampuni hiyo kumerahisisha
upatikanaji wa taarifa mpya kwa wakati zinazojiri kote nchini na hata nje ya
nchi kupitia simu na kompyuta mpakato zinazotumia mtandao wa Vodacom.
Kwa mujibu wa katibu tawala
huyo aliipongeza kampuni ya Vodacom kwa uamuzi wake wa kufungua duka hilo mjini
Masasi litakalotoa huduma kwa wananchi wote wa wilaya ya Masasi na wale wa
wilaya za jirani ikiwemo wilaya ya Nanyumbu huku akitoa wito kwa wananchi
wilayani humo kuunga mkono jitihada za serikali kupitia makampuni binafsi
katika kukuza sekta ya mawasiliano.
Kwa upande wake meneja
mauzo wa kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom wilaya ya Masasi Angetile Martin alisema ufunguzi wa duka hilo wilayani
Masasi ni moja ya hatua nzuri kwa kampuni hiyo katika kwafikia watanzania wote
ili kupunguza kadhia ya wateja ya kufuata huduma kwa umbali mrefu kutoka kwenye
maeneo wanayoishi.
Alisema huduma mbalimbali
zitapatikana kwenye duka hilo la kisasa la kampuni hiyo mjini Masasi zikiwemo
modem zenye kasi kubwa,simu za mkononi,huduma ya kuweka na kutoa pesa kote
nchini kupitia huduma ya M-Pesa pamoja
na huduma za M-Pawa na kwamba wamejipanga kutoa huduma nzuri kwa wateja wao.
Alisema kwa wilaya ya
Masasi idadi ya wateja ni kubwa mazingira yaliyosababisha kampuni ya Vodacom
kuanzisha duka hilo na kwamba lengo ni kutoa huduma bora kwa wateja popote
walipo huku akitoa rai kwa wakazi wa mji wa Masasi na vitongoji vyake
kutembelea duka hilo wezeze kujipatia bidhaa bora za kisasa.
“Kampuni yetu ya Vodacom
imejipanga kutoa huduma bora za kisasa kwa watanzania wote…na lengo letu ni
kuhakikisha kila mtanzania popote alipo anatumia huduma zetu za Vodacom ambazo
kwa sasa ni bidhaa bora ukilinganisha na makampuni mengine ya simu”.alisema
Angetile.
Aidha Vodacom kwa sasa
inatoa huduma ya kifaa chenye uwezo wa hali ya juu ambacho kwa lugha ya kitaalamu huitwa Vodacom
Router chenye uwezo wa kutumia intanenti bila ya kutumia waya huku kikiwa na
uwezo wa kutumiwa na watumiaji wa kompyuta zaidi ya kumi kwa wakati mmoja.
Mteja akiangalia simu ndani ya duka hilo la Vodacom hii leo mara baada ya kuzinduliwa rasmi.mbele yake ni wafanyakazi wa kampuni hiyo ya Vodacom.
Katibu Tawala wilaya ya Masasi Danford Peter akikata utepe kushiria uzinduzi wa duka la kampuni ya simu nchini ya Vodacom lililozinduliwa hii leo mjini Masasi.
Katibu Tawala wa wilaya ya Masasi Danford Peter akifurahia jambo wakati anazungumza na mmoja wa wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom (hayuko pichani) ndani ya duka hilo baada ya kulizinduz rasmi.
Wafanyakazi wa kampuni ya Vodacom tawi la Masasi wakiwa kwenye picha ya pamoja na katibu tawala wa wilaya ya Masasi Danford Peter ndani ya duka la kampuni hiyo mjini Masasi mara baada ya uzinduzi rasmi.
Wafanyakazi wa Vodacom wakiwa kwenye picha ya pamoja na mgeni rasmi ambaye ni katibu tawala wa wilaya ya Masasio Danford Peter nje ya duka hilo.
Duka la kisasa la kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom lililozinduliwa hii leo mjini Masasi likiwa linaonekana kwa nje duka hilo lipo eneo la Masasi Mbovu.
DUKA hilo la Vodacom linavyoonekana kwa ndani
MENEJA mauzo wa kampuni ya Vodacom wilaya ya Masasi Angetile Martin akimpa maelezo katibu tawala wa wilaya ya Masasi Danford Peter nje ya duka la vodacom kabla ya duka hilo kuzinduliwa hii leo mjini Masasi.
KATIBU Tawala wa wilaya ya Masasi Danford Peter akikata utepe
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD