TANGAZO
Na Christopher
Lilai,Nachingwea,
Wananchi
wilayani Nachingwea,mkoani Lindi wameombwa kuwa makini katika kufanya maamuzi
sahihi ya kuwapata viongozi watakaoiongoza nchi kwa kuchambua sifa za viongozi
wanaowania nafasi mbalimbali za uongozi na si kufuata
mkumbo.
Hayo
yalisemwa na Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Lindi,Amiri Mkalipa wakati
wa uzinduzi wa Kampeni za Chama cha Mapinduzi wilayani humo
yaliyofanyika kwenye viwanja vya Mauridi mjini hapa.
Alisema
wananchi wanapaswa kuwa makini huku akiwaomba kutoyumbishwa na maneno ya
baadhi ya watu yanayosema ya kuwa CCM
haijafanya chochote ndani ya kipindi chake chote cha utawala.
Alisema kwa kipindi cha miaka kumi ya uongozi wa Rais
Jakaya Kikwete ameweza kuboresha huduma za kijamii ikiwemo
miundombinu ya Barabara,elimu afya kilimo na maji.
Akihutubia
kwenye uzinduzi huo Mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la Nachingwea
Hasani Masala alisema kilichomsukuma kuwania nafasi hiyo ni kuwatumikia
wananchi wa wilaya hiyo na Tanzania kwa ujumla huku akisisitiza kutilia
maanani suala la elimu kwa ngazi zote na kwa ubora unaostahili kwa
kuwa na walimu wanaotosheleza.
Alibainisha
kuwa kwa kipindi cha uongozi wake atahakikisha anaisimamia halmashauri ya
wilaya ili iweze kuongeza mapato bila ya kuwagandamiza wananchi na
udhibiti wa matumizi ya mapato hayo.
“Nimeifanyia
kazi wilaya ya Nachingwea ndani ya halmashauri takribani
miaka 12 naifahamu si kwa kusoma kwenye vitabu naijua
vizuri kwa kusimamia nidhamu ya matumizi”.alisema Masala.
Kwa
mujibu wa Masala alisema atahakikisha kilimo kinaboreshwa kwa kuongeza zana za
kisasa ikiwemo matrekta na kuwa pia atasimamia kwa ukaribu kuona
wakulima wananufaika na mfumo wa ununuzi wa mazao wa stakabadhi ghalani na kuwa hatokubali kuona
wakulima wakishindwa kunufaika na mazao yao hasa zao la korosho.
Kwa
upande wa vijana wa Boda boda Masala aliwaomba kutotumika vibaya na
wanasiasa ambao wana lengo la kujipatia uongozi kupitia wao na
baadae kuwatelekeza na matatizo yao.
Aliwaomba
kutotumika kama vijiko kwani nchi ikikabidhiwa kwa viongozi wasio na uadilifu watakaoathirika zaidi
ni wao na vizazi vyao hivyo ni vyema wakafanya maamuzi ambayo
yataisaidia nchi badala ya kuiangamiza kwa kutumia vibaya fursa ya sanduku la
kura.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD