TANGAZO
MGOMBEA wa nafasi ya Ubunge jimbo la Ndanda,wilaya ya Masasi mkoani Mtwara Mariam Reuben Kasembe akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni uliofanyika leo katika kijiji cha Nanganga wilayani Masasi ambapo amewaomba wananchi wa jimbo hilo wamchague aweze kuwatumikia.
MJUMBE wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi wilaya ya Masasi Ramadhani Pole (kulia) akiwa anafuatilia kwa makini maelezo ya ufunguzi wa kampeni za chama hicho kwa jimbo la Ndanda kutoka kwa mwenyekiti wa CCM wilaya ya Masasi Kazumari Malilo(hayupo pichani) kulia kwake ni mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la Ndanda Mariam Reuben Kasembe.
MWENYEKITI wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Masasi Mzee Kazumari Malilo (Simba wa Yuda) akihutubia maelfu ya wanachama wa chama hicho pamoja na wananchi waliojitikeza kwenye uzinduzi wa kampeni za chama hicho zilizofanyika hii leo kijijini Nanganga Masasi.
WANACHAMA wa CCM wakicheza ngoma kwenye sherehe za uzinduzi wa kampeni za chama hicho kwa jimbo la Ndanda mkoani Mtwara.
KATIBU wa chama cha mapinduzi mkoa wa Mtwara Shaibu Akwilombe akimnadi mgombea wa nafasi ya ubunge jimbo la Masasi Mariam Kasembe pamoja na madiwani wa kata kwenye jimbo hilo la Ndanda hii leo kwenye kijiji cha Nanganga wilayani Masasi.
Shaibu Akwilombe katibu wa CCM mkoa wa Mtwara akizungumza na wananchi wakati wa mkutano wa uzinduzi wa kampeni za chama hicho hii leo katika kijiji cha Nanganga ambapo amewataka watanzania kuichagua CCM.
MGOMBEA wa nafasi ya Udiwani kata ya Nanganga kwa tiketi ya chama cha mapinduzi Hamza Ramadhani Kitambi akiomba kura kwa wana CCM pamoja na wananchi wa kata hiyo kwenye uchaguzi mkuu ujao ili aweze kuwaletea maendeleo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD