TANGAZO
MADEREVA Bodaboda wilayani Masasi wametakiwa kuanzisha umoja wao ambao utawasaidia katika matukio mbalimbali yatokanayo na vyombo vya usafiri wanavyotumia.
Rai hiyo imetolewa leo na katibu Tawala wa Wilaya ya Masasi Danford Peter wakati anafungua mafunzo ya siku saba kwa madereva bodaboda wa wilaya ya Masasi.
MRATIBU wa Mafunzo kutoka Future World Vocational Institute David Mkenza akiwaonesha Madereva Bodabaoda wa wilaya ya Masasi moja ya ishara zinazotumika Barabarani na polisi wa Usalama Barabarani ambazo nyingio kati ya hizo madereva wengi hawazifahamu.
MADEREVA Bodaboda wakitoa ishara kuashiria kuwa wako tayari kufuata sheria na kanuni za Usalama Barabarani hii leo kwenye Ukumbi wa Miduleni Halmashauri ya wilaya ya Masasi.
Wakiimba Wimbo Maalumu wa Kumkaribisha Mgeni Rasmi ambaye ni katibu Tawala wa Wilaya ya Masasi Danford Peter.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Wilaya ya Masasi Azaria Makubi wakati anazungumza na waendesha Bodaboda (Hawapo Pichani) kabla ya ufunguzi wa mafunzo ya siku saba kwa madereva hao.
MKUU wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Wilaya ya Masasi Afande Nicodem akimkaribisha mkuu wa jeshi la Polisi wilaya ya Masasi kuzungumza na madereva Bodaboda hii leo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD