TANGAZO
Na
Clarence Chilumba.
WAISLAMU nchini
wametakiwa kuwa na umoja na mshikamano miongoni mwao huku wakikumbushwa
kuitumia ibada ya Hijja kama somo la umoja kwa waislamu katika kutii sheria za
dini,kupanga mikakati thabiti ya maendeleo pamoja na kuaminiana mionogoni mwao.
Pia wameaswa kuacha
chuki zisizo na maana na mitazamo tofauti kwa kuwa wote wanamuabudu mungu mmoja tu na
ndio maana hata kwenye ibada ya Hijja waislamu wote huimba na kusali sala moja
na kwamba hakuna mtu yeyote anayeweza
kutambua kwenye halaiki hiyo nani muislamu na yupi si muislamu.
Wito huo umetolewa leo
na sheikh Salum Msabah Mbaruok wakati anatoa
mada kwa umma wa waislamu wa Ole Kianga Pemba huko Zanzibar kwenye Hijitimai iliyorushwa moja kwa moja na kituo cha
televisheni cha ZBC2 ambapo alisema hata mtume Muhamad S.A.W alisisitiza umoja
wa waislamu huku akikiri kuwa waislamu wa sasa ulimwenguni wamekuwa wakienenda
kinyume na mafundisho ya mtumu Muhamad.
“Hata Nyuki kwenye
masega yao wanajitambua kuwa ni umma mmoja kuliko sisi waislamu hivyo ni vyema waislamu tukawa kitu kimoja… hata hawa
waislamu wa asili ya Asia hasa Wahindi ni dhahiri kuwa wana ubaguzi na mfano ni
mimi nimewahi kubaguliwa hadharani nikiwa darasani na mtoto wa kiarabu huko Saudi
Arabia”.alisema Sheikh Mbaruok.
Alisema kwa sasa kote
ulimwenguni kumekuwa na ongezeko kubwa
la misikiti na kwamba hiyo yote inatokana na ubaguzi ambao waislamu wengi wamekuwa
wakibaguana wenyewe k wa waislamu.
Kwa mujibu wa Sheikh
Mbaruok alisema tatizo waislamu hawaitumii ibada ya wa wenyewe na kwamba wakati
umefika kwa sasa wa kuzungumzia mifarakano iliyopo miongoni mwa waislamu.
Hijja kama somo kwao na ndio maana wanaporejea
kutoka kwenye ibada hiyo bado toauti zinakuwepo ikiwemo tofauti wakati wa
kuswali,maulidi,wakati wa mfungo wa Ramadhani na nyinginezo nyingi ambazo kwa
hakika hazipaswi kuachwa zikiendelea.
Alisema dini zote
zimekuja zikiwa na lengo la kudumisha umoja,upendo na mshikamano miongoni mwa
wanadamu lakini kwa sasa hali ni tofauti kwani dini zimegeuzwa kuwa kama
kichocheo cha malumbano ya kidini na hata wengine wamekuwa wakiitumia vibaya
dini kuhusisha na masuala ya kisiasa.
“Umoja hujengwa kwa
kutumia hekima bila hekima hatuwezi kujenga umoja wetu nchini hivyo nawaomba
waislamu wenzangu amani hii tuliyonayo hatupaswi kuichezea…hebu angalieni
mifano mbalimbali ya nchi zilizopo kwenye vita zingine zikiwa ni za ndani ya
bara letu la Afrika ambazo wananchi wake
wamekuwa wakimbizi wa kivita”.alisema.
Alisema waumini wa
mwanzo wa dini wa kiislamu walifuata mafundisho ya manabii wa mwanzo lakini hii
leo hali imekuwa tofauti kabisa huku akitoa mfano hasa kwenye muandamo wa mwezi
kumekuwa na mgogoro mkubwa sana miongoni mwa waislamu huku wengine wakienda
mbali na kusema kuwa wapo waislamu hudai kuwa wenzao wamekuwa wakifunga
Ramadhani kwa kufuata mwezi wa SMZ kitu ambacho si kweli.
Aidha alisikitishwa na
baadhi ya waumini wa kiislamu ambao wamekuwa wakiwakosoa wenzao kuwa hata
mavazi wanayovaa hayaendani na imani ya dini hiyo kwa sababu ya kanzu zao
kufunika viatu ambapo aliwaomba waumini waache tofauti zao kwa lengo la kujenga
uislamu kama walivyofanya maimamu waliopita.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD