TANGAZO
Mh. Bernard Kamillius Membe alizaliwa tarehe 09 Novemba 1953
katika Kijiji Cha Rondo – Chiponda kilichopo katika Wilaya ya Lindi Vijijini
mkoani Lindi. Alizaliwa kwa mzee Kamillius Antony Ntanchile na mama Cecilia
Josha Membe.
Mh. Membe ni mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Mtama kupitia (CCM)
toka mwaka 2000 na ni waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa toka
mwaka 2007.
HISTORIA YA ELIMU
YAKE:
Mh. Membe alipata elimu ya msingi katika Shule ya Rondo –
Chiponda, elimu ya sekondari (O-Level) katika seminari ya Namupa na elimu ya
kidato cha tano na sita katika seminari ya Itaga.
Mh. Membe alipata elimu ya Chuo Kikuu katika vyuo vya Mlimani
(UDSM) Shahada ya kwanza (BA) na Johns Hopkins Marekani kwa shahada ya pili
(MA).
Mh. Membe ni mtaalamu wa Maswala ya Usalama, aliyosomea huko
Uingereza (UK) na Maswala ya Sayansi ya siasa aliyosomea kivukoni
Dar-es-salaam.
UZOEFU KATIKA
SIASA NA UONGOZI KIUJUMLA:
Historia ya uongozi ilianzia pale alipokuwa mchambuzi wa Masuala
ya Usalama wa Taifa katika ofisi ya Rais, na baadae alipoteuliwa kuwa mshauri
wa Balozi wa Tanzania nchini Canada.
Nafasi alizowahi kutumikia ni:-
·
Mchambuzi wa
Masuala ya Usalama wa Taifa.
·
Mshauri wa Balozi.
·
Naibu waziri wa
Mambo ya Ndani.
·
Naibu waziri wa
Nishati na Madini.
·
Waziri wa Mambo ya
Nje na Ushirikiano wa Kimataifa.
Familia yake:
Mh. Membe alifunga ndoa na Dorcas Richard Masanche (1986),
pamoja wamebahatika kupata watoto wa kiume wawili na wakike mmoja.
Katika hatua nyingine Wananchi wengi walioongea na Blog ya Mtazamo Mpya
wanaonekana kukubaliana kuwa Membe
anatisha kwa CV nzuri inayofaa kwa Rais wa nchi ya Tanzania amesoma mambo ya
uongozi na utawala, usalama wa taifa na inteligensia, usuluhishi, mambo ya nje
na mahusiano ya kimataifa; amefanya kazi ya intelijensia kwa muda mrefu, zaidi
ya miaka 10 na amepanda sana vyeo ndani ya idara hiyo nyeti na hivyo anazijua
siri nyingi za serikali na namna nzuri ya kuongoza nchi;
ameshika nafasi ya ukatibu wa mambo ya nje ndani ya chama chake
- ccm kwa zaidi ya miaka mitano na hivyo amekaa kamati kuu kwa muda kidogo
akishuhudia na kushiriki maamuzi nyeti ya uongozi wa nchi kupitia chama tawala
yakifanywa; amekuwa waziri wa mambo ya nje kwa zaidi ya miaka minne sasa,
amekuwa afisa wa balozi yetu ya Canada.
Aidha Mheshimiwa Membe ameshiriki kama mtu wa karibu sana wa
kampeni zilizomwingiza Rais JK madarakani - kwa haya tu utaona ni mtu ambaye
kama ataamua, ama kama anavyopenda kusema yeye mwenyewe kuwa 'ataoteshwa'
kuwania Urais ataweza kuwa na wasifu wa kutosha zaidi kuliko wengine
waliojitokeza ama wanasemwa semwa sana na watanzania walio wengi.
Zaidi ya hayo, Membe amekuwa mshauri wa karibu sana wa Rais
Kikwete na mratibu wa mambo yetu ya nje ya nchi kuliko wote waliojitokeza ama
wanasemwasemwa, na hana kashfa za rushwa wala ubadhirifu wa mali ya umma kama
wenzake.
Pia afya yake inaonekana kuwa imara na yuko kwenye umri muafaka
kabisa kuwa Rais. Kwa mujibu wa katiba ambayo si rasmi lakini inafuatwa na
Tanzania hii ni zamu ya Rais kuwa ni muumini wa dini ya kikristo, Membe ni
mkristo mzuri kabisa na mwenye kufuata misingi ya dini yake na dhehebu lake na
hivyo anatimiza sifa kabisa.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD