TANGAZO
Bwana Shaibu Athumani (35) muathirika wa Mamba |
Na Clarence
Chilumba, Masasi.
SERIKALI kupitia
wizara ya maliasili na utalii imesema iko tayari kutoa vibali kwa maofisa wake
wa idara ya wanyamapori vya kuvuna mamba kwenye maeneo ambayo wananchi wake
wamekuwa wakiuawa au kujeruhiwa na wanyama hao waishio majini.
Kauli hiyo yenye
matumaini kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya mito ikiwemo mto Ruvuma
wilayani Masasi imetolewa leo na waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu
wakati anazungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Manyulli na
Mnavira kata ya Mnavira Halmashauri ya wilaya ya Masasi wakati wa ziara yake wilayani humo.
Ziara hiyo ya
waziri Nyalandu imekuja baada ya malalamiko ya muda mrefu kutoka kwa wananchi hao
ambao wamekuwa wakipoteza viungo vyao huku wengine wakipoteza maisha kutokana
na ongezeko la mamba katika mto Ruvuma mpakani mwa Tanzania na Msumbiji
kikiwemo kitongoji cha Mdohe kijiji cha Manyuli.
Alisema serikali imelazimika
kuchukua hatua hizo kutokana na wanyama hao kujeruhi na kuua watu na kwamba
zoezi hilo la uvunaji wa mamba hao utafuata kanuni na taratibu zilizopo huku
akiweka wazi kuwa ofisa wa wanyamapori nchini atakayetumia vibaya kutolewa kwa
vibali hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema si busara
kuacha wananchi wakiendelea kupoteza maisha wakati serikali ikiona na kwamba
hatua hiyo inaonesha ni kwa jinsi gani serikali ya chama cha Mapinduzi
inavyowajali wananchi wake.
Katika hatua
nyingine jana waziri wa maliasili na utalii amekabidhi hundi zenye thamani ya
shilingi 1,800,000 kwa wananchi wa wilaya ya Masasi wapatao 62 ambao kwa
nyakati tofauti walijeruhiwa na wengine kupoteza viungo ma maisha yao ikiwa
kama fidia kwao kwa matatizo hayo.
Akikabidhi hundi
hizo kwa katibu tawala wa wilaya ya Masasi Danford Peter, waziri wa maliasili
na utalii Lazaro Nyalandu alisema fidia hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa ahadi
ya serikali kwa wananchi wa vijiji vya Manyuli na Mnavira walioathirika na
mamba hao waishio mto Ruvuma.
BWANA Rashid Thabiti Ngwalu (56) ni miongoni mwa wananchi wa kijiji cha Mnavira ambao wameathirika kutoaka na Mamba ambapo kwa upande wake yeye amepoteza korodan zake zote mbili.
WAZIRI wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu akimwelekeza jambo Diwani wa kata ya Mnavira Ramadhani Chilumba wakiwa Mto Ruvuma hii leo asubuhi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD