TANGAZO
Na Bashiru Kauchumbe Ruangwa.
JUMLA ya kaya 6,804 katika wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi zimenufaika na mpango wa kunusuru kaya maskini unaotekelezwa
na Mfuko wa maendeleo ya jamii nchini (TASAF-III).
Hayo yalisemwa jana na Mratibu wa TASAF Wilaya ya Ruangwa Mwajuma
Salumu wakati anaongea na Blog ya Mtazamo Mpya ofisini kwake.
Alisema hadi sasa wilaya hiyo imeshafanya uhawilishaji wa fedha
kwa kaya maskini kwa awamu nane ambapo zaidi
ya shilingi milioni 179 zimetumika kwa walengwa wa mpango huo wilayani
humo.
Alisema lengo la mpango huo wa TASAF III ni kuziwezesha kiuchumi
kaya maskini na zile zinazoishi katika mazingira hatarishi ili ziweze kupata
huduma muhimu za kijamii zikiwemo
chakula,afya,elimu pamoja na
fursa za kujiongezea kipato.
Kwa mujibu wa mratibu huyo wa TASAF Wilaya ya Ruangwa alizitaja
baadhi ya changamoto zinazosababisha
utekelezaji wa mradi huo kusuasua kuwa
ni upungufu wa hasa wakati wa uhawilishaji rasilimali fedha kwa walengwa
pamoja na baadhi ya wanasiasa kuingilia
utendaji hasa uteuzi wa kaya zilizopo katika mazingira magumu ambapo wengi wao wamekuwa
wakishinikiza kuingizwa kwenye mpango kaya ambazo hazina vigezo.
Zaituni Abdallah na Rashidi mpekeyo ni baadhi ya wanufaika wa
mpango huo katika vijiji vya Mkutingome
na Chingumbwa ambao waliipongeza
serikali kwa kuanzisha mpango huo ambao umekuwa ni mkombozi kwa kaya maskini
nchini.
Walisema baadhi yao wamenufaika kwa kiasi kikubwa kupitia mpango
huo tangu ulipoanza huku wakikiri kuwa fedha hizo zimewasaidia ulipa karo za
watoto wao shuleni,kuanzisha ufugaji wa kuku pamoja na kuwekeza katika kilimo.
Kwa upande wake Hakika Hussein mkazi wa Kijiji cha Mkutingome alisema wapo baadhi ya watu wanaoukosoa utaratibu huo
wa uhawilishaji rasilimali fedha kwa kaya maskini kwa kuhusisha na masuala ya kisiasa hasa kipindi hiki kinachoelekea kwenye uchaguzi wakidai kuwa ni
kampeni kutoka kwa chama tawala CCM ili kiendelee kushika hatamu.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD