TANGAZO
Bwana Chatoni Rashidi Chatoni. |
Wananchi waishio katika Halmashauri ya Mji wa Masasi Mkoani Mtwara hii leo wamejitokeza kwa wingi tangu alfajiri kwanye vituo vya kujiandikisha wakati wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Zoezi
hilo ambalo kwa Halmashauri ya Mji wa Masasi limeanza katika kata za
Mtandi,Jida,Chanikanguo pamoja na Mkuti na ambalo litadumu kwa muda wa siku
saba(7) ili kuwezesha wananchi wote wa kata hizo kuweza kujiandikisha ili
wapate sifa za kushiriki kwenye uchaguzi mkuu ujao pamoja na zoezi la kuipigia
kura ya ndio au hapana katiba inayopendekezwa.
Akizungumza
na Blog ya Mtazamo mpya hii leo majira ya saa 2:10 Asubuhi Chatoni Rashidi
Chatoni ambaye ni mwananchi wa kwanza kuandikishwa katika kituo cha JIDA kata
ya Jida Halmahauri ya mji wa Masasi alisema vitambulisho hivyo vipya viko
tofauti na vile vya awali na kwamba ameipongeza tume ya Taifa ya uchaguzi kwa
uamuzi wa kuleta mfumo mpya wa kupata vitambulisho vya wapiga kura.
Nao
baadhi ya waandikishaji wasaidizi wa zoezi hilo pamoja na BVR Operator walisema
kuwa kwa ujumla zoezi linaenda vizuri licha ya kuwepo kwa baadhi ya changamoto
ambazo walikiri kuwa zimekuwa zikipatiwa ufumbuzi wa haraka kutoka kwa
wataalamu wa mifumo kwa ngazi ya Halmashauri ya mji wa Masasi kwa ushirikiano
na wale wa kutoka tume ya Taifa ya uchaguzi.
Wananchi wa kituo cha JIDA wakiwa kwenye misururu mirefu wakisubiri kujiandikisha kwenye zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa kutumia mfumo wa kuchukua au kupima taarifa za mwili (Physiological) au tabia ya mwanadamu na kuzihifadhi katika kanzi (Database) kwa ajili ya utambuzi. (BVR).
MKUU wa wilaya ya Masasi Bernald Nduta akiweka vidole gumba vyake kwenye mashine ya BVR kwa lengo la utambuzi wa taarifa zake wakati wa zoezi la mfano kwa waandishi wasasidizi wa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
MKUU wa Wilaya ya Masasi Bernald Nduta akiweka saini kwenye mashine ya BVR wakati wa zoezi la majaribio hapo jana kwenye ukumbi wa sekondari ya wasichana Masasi.
BVR OPERATOR Grasha Sanga (Kulia) Akipeana mkono na mkuu wa wilaya ya Masasi Bernald Nduta (kushoto) baada ya kumkabidhi kadi yake ya mfano.Anayeshuhudia tukio hilo ni ofisa wa uchaguzi Halmashauri ya mji wa Masasi Shaibu Mwakatika.
Viongozi wa vyama vya siasa wilaya ya Masasi waliokuja kushuhudia zoezi la ufangwaji wa mafunzo kwa waandishi wasaidizi yaliyofanyika kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Masasi.
MWENYEKITI wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Masasi Kazumari Malilo akiweka saini ya vidole gumba kwenye mashine ya BVR wakati wa mazoezi ya vitendo kwa waandishi wasaidizi na BVR Operator.
Mzee Malilo akikabidhiwa kadi yake ya mfano kutoka kwa mwandishi msaidizi
MWENYEKITI wa Chama Cha Wananchi (CUF) Wilaya ya Masasi Yusuph Matola aliyekaa (kushoto) akijibu maswali kutoka kwa mwandikishaji msaidizi kuhusu taarifa zake wakati wa zoezi la mafunzo kwa vitendo kwa waandishi hao.
Bwana Chatoni Rashidi Chatoni akiwa ameshikilia kitambulisho chake kipya mara baada ya kukamilisha zoezi la kuandikishwa kwa kutumia mfumo wa BVR.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD