TANGAZO
Na Clarence Chilumba.
Mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la
Safina Kombo (33) mkazi wa kijiji cha Luchelegwa kata ya Luchelegwa Halmashauri
ya wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi amefariki dunia papo hapo baada ya kugongwa na lori aina ya
Scania mali ya kampuni ya Mohamed Enterprises akiwa amepakiwa kwenye pikipiki
aina ya SanLg iliyokuwa ikiendeshwa na Hamis Ndaka (55)
Tukio hilo limetokea jana majira ya saa
2:00 usiku katika maeneo ya kijiji cha Mwena kilichoko Halmashauri ya wilaya ya
Masasi jirani na eneo la burudani lijulikanalo kwa jina la Kill Pub walipoenda
kumalizia pasaka.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo
Ofisa mtendaji wa kata ya Luchelegwa Said Ng’itu alisema tukio hilo la
kusikitisha limemuhusisha mke wa mtu bwana Obote Muhidini (40) aliyekuwa na
mpenzi wake Hamis Ndaka ambaye ni mwandishi wa chama cha msingi cha Luchelegwa.
Alisema jana asubuhi marehemu
alimuaga mume wake kuwa anaelekea Ndanda kwa ajili ya kupata dawa kutokana na
matatizo ya afya yaliyokuwa yanamsumbua huku taarifa za ndani zikonesha kuwa
hakwenda kwa ajili ya kuchukua dawa bali ni kwa lengo la kuonana na mpenzi wake
eneo la Kill Pub lililopo katika kijiji cha Mwena-Ndanda.
Kwa mujibu wa ofisa mtendaji huyo
alisema baada ya kukamilisha unyama wao waliamua kuondoka kurudi nyumbani
lakini baada ya kutoka kwenye eneo hilo la Bar walipata ajali ya kugongwa kwa
nyuma na lori hilo lililokuwa likielekea Masasi.
Tayari mwili wa Marehemu umeshazikwa
hii leo majira ya saa 10:00 jioni katika makaburi yaliyopo katika kijiji cha
Luchelegwa wilayani Ruangwa Lindi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD