TANGAZO
Na Clarence
Chilumba,Mtwara.
Jumla ya kaya
zipatazo 44,545 mkoani Mtwara zilizopo katika
mpango wa kunusuru kaya maskini sana zimenufaika na mpango huo unaotekelezwa na
mfuko wa maendeleo ya jamii nchini TASAF III.
Aidha kila kaya
iliyopo kwenye mpango huo hupatiwa
ruzuku kila baada ya miezi miwili na kwamba hadi sasa mkoani Mtwara jumla ya
ruzuku tano zimetolewa ambapo hadi novemba 2014 zaidi ya shilingi bilioni sita zilipokelewa kwa ajili ya utekelezaji wa
mpango huo.
Akizungumza
katika mahojiano maalumu na "Blog ya Mtazamo Mpya" mratibu wa TASAF mkoa wa Mtwara Monica Mahundi alisema
mpango huo wa kunusuru kaya maskini una
lengo la kuongeza kipato,fursa na uwezo wa kugharamia mahitaji muhimu kwa kaya
hizo.
Alisema
halmashauri ya Mtwara-Mikindani ni moja
ya Halmashauri inayotekeleza mpango wa kunusuru Kaya Maskini ambao hadi sasa
mpango huo umetekelezwa katika mitaa 34 na vijiji
viwili huku jumla ya miradi 39 ikiibuliwa na kutekelezwa.
Kwa
mujibu wa mratibu huyo wa mkoa alisema zoezi
la utekelezaji wa miradi Katika halmashauri hiyo lilianza januari mosi 2015
likiwahusisha walengwa wote walioibuliwa kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini
kwa kila ngazi ya vijiji na mitaa mkoani humo.
Alisema
jumla ya shilingi 183,264,352,000 zimetumika katika
utekelezaji wa miradi hiyo 39 inayotekelezwa na TASAF ambapo
shilingi 183,264,000 ni fedha za walengwa huku jumla ya shilingi 61,088,000 zikiwa ni fedha za usimamizi wa utekelezaji wa miradi katika ngazi ya
Halmashauri na ngazi ya Jamii.
Alisema
Miradi hiyo inalenga kuinua na kuboresha kipato cha kaya kupitia ushiriki wa walengwa kwa kufanya kazi
katika siku 15 za mwezi na kwamba hadi sasa walengwa hao wameshalipwa katika kipindi cha mwezi Januari,Febuari pamoja na Machi.
Mahundi
alizitaja changamoto zilizopo mkoani humo katika utekelezaji wa miradi iliyopo
katika mpango wa kunusuru kaya maskini ikiwemo fedha za walengwa kutofika kwa wakati hivyo kusababisha
malalamiko makubwa wanayoyapata waratibu wa mpango kutoka kwa walengwa.
Changamoto
zingine ni kwa baadhi wa walengwa kukataa kushiriki katika kufanya kazi katika
miradi ya ajira muda pamoja na vijiji na
mitaa mingi mkoani humo kuwa na fedha
kidogo ya usimamizi hivyo kushindwa kufikia gharama halisi ya fedha za
usimamizi wa miradi.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD