TANGAZO
SHIRIKA linaloshugulikia idadi ya watu
duniani (UNFPA) limetoa msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya Sh.389 milioni
katika hospitali ya wilaya ya Newala mkoani Mtwara pamoja na chuo cha uuguzi na
ukunga kilichopo wilayani humo lengo ni kupanua huduma za afya ikiwa ni pamoja
na kupunguza idadi ya vifo vya akina mama wajawazito pindi wanapojifungua.
Msaada
huo umetolewa jana na Mwakilishi mkazi hapa nchini wa shirika la UNFPA ,Felista
Bwana ambaye alimwakilisha Mwakilishi mkuu mkazi wa shirika hilo Natalia Kashem
ambapo Bwana alisema kuwa lengo la kutoa msaada huo ni kupanua wigo wa utoaji
wa huduma za afya nchini hasa za mama na mtoto.
Alisema
shirika limechukua hatua hiyo kutokana na kuwepo kwa idadi kubwa ya vifo vya
akina mama wajawazito pindi wanapojifungua na watoto waliochini ya umri wa
miaka mitano ambapo vifo hivyo hujitokeza kutokana na ukosefu wa vifaa tiba
ambavyo havina viwango vya kukabiliana na tatizo hilo.
Aliongeza
kuwa vilivyotolewa ni vitanda vya kujifungulia akina mama,vitanda maalumu vya
kutunzia watoto ambao wamezaliwa wakiwa na uzito mdogo(NJITI) pia na watoto
wenye matatizo ya kushindwa kupumua pamoja na vifaa vya upasuaji na kurekebisha
mfumo wa utoaji ganzi ambapo vifaa hivyo vinathamani ya Sh.65 milioni.
Bwana
alisema kupitia vifaa hivyo anaamini kwamba itakuwa suluhisho la akina mama na
watoto kuendelea kupoteza maisha ambapo hapa nchini tatizo hilo limekuwa kama
janga la kitaifa ambapo shirika hilo limeamua kuongeza kasi ya kupunguza vifo
kwa kutoa msaada wa vifaa tiba katika hospitali mbalimbali hapa nchini.
Aidha
Mwakilishi huyo alikabidhi vifaa mbalimbali vya Maabara ya kujifunzia ikiwemo
vitabu na vifaa tiba vyenye thamani ya Sh.324 milioni ambapo jengo la Maabara
hiyo pia limezinduliwa rasmi na mkurugenzi wa mafunzo na maendeleo ya
rasilimali watu kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii Dkt. Otilia Gowelle
ambaye aliongozana na viongozi hao wa UNFPA.
Kwa
upande wake mganga mkuu wa hospitali hiyo ya wilaya ya Newala kwa niaba ya
mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo,Dkt.Yudas Ndungile alilipongeza
shirika hilo kwa kutoa msaada huo wa vifaa tiba pamoja na kufadhiri ukarabati
wa jengo la Maabala ya kujifunzia katika chuo cha uuguzi na ukunga wilayani hapa.
“Msaada
huu wa vifaa tiba umekuja kwa wakati muhafaka kwani wilaya yangu inakabiliwa na
changamoto kubwa ya vifaa tiba hasa katika wodi ya uzazi na kwenye chumba
upasuaji ambapo kwa sasa tatizo litakuwa limepungua baada ya kupata msaada huu
muhimu kwetu,”alisema Dkt.Ndungile
Alisema
mfano katika hospitali yake baadhi ya akina mama pamoja na watoto hupoteza
maisha kutokana na tatizo la ukosefu wa vifaa tiba hivyo kupitia vifaa hivyo
vitasaidia kuondoa tatizo la vifo katika hospali hiyo.
Mwisho.
Mwakilishi wa UNFPA nchini Felista Bwana akikabidhi msaada wa vifaa kwa mganga mkuu wa Hospitali ya wilaya ya Newala Mkoani Mtwara DKT. Yudas Ndungile.
Baadhi ya Wanachuo wa Chuo Cha Uuguzi katika chuo kilichopo katika Hospitali ya Wilaya ya Newala Mkoani Mtwara wakifuatilia hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa katika hospitali hiyo.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD