Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

MBARONI KWA KUKUTWA AKIWA AMEVALIA SARE ZA JWTZ

TANGAZO
Na Fatuma Maumba,Mtwara.
Jeshi la Polisi mkoani Mtwara linamshikilia Daudi Innocent (31) mlinzi wa kampuni ya Naf Security kwa kukutwa akiwa amevalia sare za jeshi la wananchi wa Tanzania kinyume na sheria.

Akizungumza na waandishi wa habari hii  leo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Augustine Ollomi, alisema tukio hilo lilitokea machi 24 mwaka huu, majira ya saa 10:00 jioni maeneo ya stendi kuu ya mabasi wilaya na mkoa wa Mtwara ambapo askari wa jeshi  la wananchi Tanzania no.MT/98739/PTE EPHREM (29), alimkamata mtuhumiwa huyo akiwa amevaa sare hizo wakati yeye sio askari wa jeshi hilo.

Kwa mujibu wa Kamanda Ollomi, alisema mtuhumiwa yupo polisi kwa mahojiano zaidi na atafikishwa mahakamani baada ya upelelezi kukamilika.

Aidha Kamanda Ollomi, ametoa wito kwa wananchi wote kutoa taarifa polisi ikiwa watambaini au kumtilia mashaka mtu yeyote kwani wahalifu wamekuwa wakitumia sare za majeshi katika kufanikisha adhima yao.

Hata hivyo Kamanda Ollomi, ameonya juu ya tabia za baadhi ya watu kujifanya kuwa watumishi wa sehemu fulani kwa  kuvalia sare  za sehemu husika na kwamba atakayebainika hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Mwisho.


TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top