TANGAZO
Na
Clarence Chilumba, Masasi.
Vijana
wapatao 16 wa eneo la Masasi Mbovu wilayani Masasi katika mkoa wa Mtwara
wameungana kuunda kikundi cha ubunifu na utengenezaji wa vifaa vya majumbani,
ofisini pamoja na viwandani kwa kutumia malighafi itokanayo na chuma pamoja na
aluminiamu badala ya mbao.
Kikundi
hicho ambacho hasa lengo lake kuu ni kupambana na uharibifu wa mazingira
utokanao na ukataji ovyo wa misitu kwa ajili ya kujipatia mbao pamoja na bidhaa
zingine zitokanazo na misitu na kwamba kimepewa jina la vitendo kwanza maarufu
kama vikwa.
Aidha
vijana hao wamefikia hatu hiyo ya utengenezaji wa vifaa mbalimbali kwa kutumia
chuma baada ya kuona wilaya ya masasi ni miongoni mwa wilaya mkoani Mtwara
ambazo suala la uharibifu wa mazingira utokanao na ukataji miti lipo kwa kiasi
kikubwa hali inayopelekea kuhatarisha uhai wa viumbe vitegemeavyo misitu hiyo.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na mwandishi wa habari hii mwenyekiti wa kikundi hicho cha
vitendo kwanza Maulidi Hokororo maarufu Ndege alisema wamekuwa wakitengeneza
fenicha za majumbani, maofisini pamoja na vifaa vya viwandani kwa kutumia chuma
na aluminiamu badala ya mbao ambazo husababisha uharibifu wa mazingira.
Alisema
kuwa vifaa ambavyo hutengenezwa na kikundi hicho ni pamoja na vitanda, meza, milango,
madirisha, viti vya majumbani na vile vya harusi, makabati, pamoja na mashine
mbalimbali za ufyatuaji matofali na kwamba vifaa hivyo vyote hutengenezwa kwa
chuma.
Kwa
mujibu wa mwenyekiti huyo alisema kiwanda hicho pia hurekebisha bodi za
magari,uundaji upya wa mfumo wa magari
pamoja na utenegenezaji wa madawati na mabanda yanayotumika kwa ajili ya utoaji
wa huduma za pesa kupitia mitandao ya simu.
Akizungumzia
kuhusu ni kwa namna gani wanakabiliana na uharibifu wa mazingira Hokororo
alisema serikali imekuwa ikiwalalamikia wanannchi wa maeneo mbalimbali hapa
nchini kuwa wemekuwa na tabia za ukataji misitu kwa ajili ya matumizi ya
utengenezaji wa fenicha za majumbani na kwamba wao kwa kutumia chuma katika
utengenezaji wa fenicha hizo ni dhahiri wanapambana na uharibifu wa mazingira.
Alisema
matarajio yao ni kuona jamii inabadilika na kuachana na tabia ya uharibifu wa
mazingira kwa kukata miti kwa matumizi
ya fenicha mbalimbali za majumbani na badala yake waanze kuwa na utamaduni wa
kuagiza fenicha zinazotengenezwa kwa kutumia malighafi zitokanazo na chuma
ambazo bei yake ni ya kawaida.
Aidha
matarajio mengine ni kufungua shule ya ufundi wa utenegenezaji wa vifaa hivyo,
kujiongezea kipato, kubadili mwelekeo wa vijana ambao siku zote hukaa vijiweni
pamoja na kubadilisha mtazamo na fikra za jamii kwamba si lazima wanunue
fenicha kutoka nchini china.
Alizitaja
changamoto wanazokumbana nazo katika utendaji wa kazi zao ikiwa ni pamoja na
ufinyu wa soko la bidhaa zao, ofisi za serikali na watu binafsi kuagiza vifaa
vya maofisini na majumbani kutoka Dar es Salaam ambavyo vingi kati ya hivyo
vimetengenezwa nchini china ambavyo mara nyingi huwa sio imara.
Mwisho.
Moja ya mafundi wa kikundi hicho cha Vitendo kwanza akitengeneza mlango wa chuma
Baadhi ya vifaa vilivyotengenezwa na kikundi cha VIKWA kwa kutumia malighafi ya chuma na Aluminiamu.
Kitanda cha chuma kilichotengenezwa na mafundi hao kiwandani hapo kinachouzwa kiasi cha fedha Tsh;Milioni moja.
Mr.Maulidi Hokororo (Ndege) ambaye ni mwenyekiti wa kikundi cha vitendo kwanza akiwa amekalia kiti cha kisasa ambacho kina sehemu ya kuwekea (Droo) kompyuta mpakato (LAPTOP) pamoja na Document zingine muhimu huku mbele ya kiti hiko kukiwa na meza.
Mashine ya kufyatulia matofali inayotumia umeme ni moja ya vifaa vilivyotengenezwa na kikundi hiko
Frame za madirisha ya vioo zikiwa kiwandani hapo tayari kwa matumizi yaliyokusudiwa
Moja ya vifaa vilivyotengenezwa kiwandani hapo
Mwenyekiti wa kikundi cha Vitendo Kwanza (VIKWA)
Jiko linalotumia pumba za mpunga pamoja na kinyesi cha Ng'ombe lililotenengenezwa kwa kutumia chuma
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD