TANGAZO
MASASI YATAMBA KUKAMILISHA MIRADI YAKE
YA MAENDELEO
Clarence Chilumba, Masasi.
HALMASHAURI ya mji wa Masasi mkoani Mtwara,imetengewa fedha shilingi
bilioni 1,028,820,000 kwa mwaka wa fedha 20145/2015 kutoka mfuko wa barabara
(Road Fund) kwa ajili ya matengenezo ya barabara zake ili ziweze kupitika kwa
urahisi wakati wote.
Pia Halmashauri hiyo kwa kutumia vyanzo vyake
vya mapato vya ndani tayari imeanza
ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi pamoja na
nyumba tano za wakuu wa
idara zinazojengwa kwenye eneo la Mtandi mjini hapa na
imekamilisha wodi ya wazazi ya mkomaindo.
Akizungumza mwishoni mwa wiki kaimu mkurugenzi
wa Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara,Henry Kagogoro alisema
mikakati mbalimbali imewekwa na
Halmashauri hiyo katika kukabiliana na tatizo la miundo mbinu hasa ya barabara
ambayo hapo awali ilikuwa ni kero kwa wananchi.
Alisema kimsingi Halmashauri pia imepanga kutumia fursa za wahisani wa ndani na
nje katika kujenga na kuimarisha miundombinu
yake na kwa maeneo yote ikiwemo barabara zenye ubora,huduma za afya, kilimo, elimu, mpango mzuri wa mji pamoja na uhakika wa huduma ya maji safi na
salama.
Kagogoro alisema kuwa kupitia
kiasi hicho cha fedha kilichotengwa
jumla ya km.172 za barabara za Halmashauri hiyo zinatarajiwa kutengenezwa
kwa kiwango cha changarawe pamoja na ujenzi wa madaraja na makaravati na
kwamba tayari ujenzi wa barabara hizo umeanza na uko katika hatua
inayoridhisha.
“Mkakati uliopo ni
kuimarisha miundombinu ya barabara kwa kuhakikisha kuwa zote zinajengwa na
zinakamilika kwa wakati ili kuondoa usumbufu ambao wananchi walikuwa wanaupata
hapo awali…na kwamba tayari ujenzi wa Barabara kwa kiwango
cha lami yenye urefu wa km.1.2 kutoka eneo la Tk hadi Sabasaba (Mkapa Road) kwa
kiasi kikubwa umekamilika kinachoendelea
kwa sasa ni ujenzi wa mifereji” Alisema.
Kaimu mkurugenzi huyo alizitaja baadhi ya barabara za mitaa ambazo ujenzi wake
unaendelea mjini humo ikiwa ni pamoja na
CCM hadi Rest Camp,Upanga hadi misufini ,Mkomaindo hadi Maendeleo,Wabiso hadi
Migongo shule ya msingi,barabara ya Makunda,ujenzi hadi Jida,Zahanati hadi
Naikula,Vijineno hadi kisiwani,Mkuti-Wapiwapi barabara ya magereza hadi
Rest,Anna Abdallah –liston garage pamoja na saiduna -mefu ambazo zote
zinajengwa kwa kiwango cha changarawe.
Aliongeza kuwa pamoja na jitihada hizo zote zinazofanywa na
Halmashauri wananchi pia wana wajibu wa kutunza miundombinu hiyo isiharibiwe na
kwamba hakusita kuwanyooshea kidole baadhi ya wananchi ambao wamekuwa na tabia
ya kutupa taka kwenye maeneo yaliyojengwa makalavati hali inayopelekea kuziba
kwa makalavati hayo na kusababisha maji kuharibu barabara.
Kwa mujibu wa Kagogoro alisema kwa
kuwa Halmashauri hiyo ni mpya inatarajia
hapo baadae kuanza ujenzi wa ofisi kuu, stendi kubwa ya kisasa ya mabasi pamoja na soko kuu kwa kushirikiana na
taasisi zisizo za kiserikali pamoja na wadau mbalimbali wa maendeleo ambapo
wananchi wanatarajia kunufaika kupitia miradi hiyo.
Aidha alisema
kuwa kwa sasa wanaendelea na ujenzi wa
maabara kwa shule zote za sekondari ili
kutekeleza agizo la Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete
inalozitaka shule zote za sekondari za kata
hapa nchini kuwa na maabara zenye vifaa vya kujifunzia na kufundishia.
Alisema pia
ujenzi wa nyumba ya mkurugenzi tayari umekamilika kwa kiwango kikubwa huku wodi
ya wazazi katika hospitali ya mkomaindo ikiwa tayari imeanza kutumika na kwamba
miradi kama vile machinjio ikiwa imeanza kutumika na nyumba za watumishi zikiwa
katika hatua ya ukamilishaji.
Mwisho.
MIRADI YA MAENDELEO KATIKA PICHA
UJENZI wa Barabara kwa kiwango cha lami yenye urefu wa Km.1.2
kutoka eneo la TK hadi Sabasaba maarufu Mkapa Road iliyopo mjini Masasi mkoani
Mtwara iliyojengwa kwa thamani ya shilingi 325,000,000.00 ambapo ujenzi huo
ulianza Mei 2014 na utakamilika ifikapo Desemba 31, 2014 kwa sasa kazi inayoendelea ni ujenzi wa
mifereji.
Line sita za kalavati, Sehemu ya barabara ya Mkapa iliyopo Masasi mjini.
Wodi ya wazazi hospitali ya mkomaindo Masasi inavyoonekana
kwa nyuma.
Machinjio ya kisasa iliyojengwa na Halmashauri ya mji Masasi katika eneo la Mtandi Thamani ya mradi huo ni
shilingi 73,000,000 zilizotolewa na serikali kuu ikiwa ni ruzuku ya miradi ya
maendeleo CDG. Ilianza kujengwa Septemba
2012 na kukamilika Januari 2014 mradi huo ulianza kutumika rasmi Juni
2014.
UJENZI wa nyumba tano za
watumishi wa Halmashauri ya mji Masasi mkoani Mtwara katika eneo la Mtandi
ulioanza Juni 2014 hadi tarehe 15 oktoba
2014 ujenzi uko hatua ya linta kwa
nyumba tatu na mbili hatua ya ukuta.
Sehemu ya nyumba tano za watumishi zinazojengwa na Halmashauri ya mji Masasi.
UJENZI wa nyumba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya mji Masasi ulioanza juni 2014 na hatua iliyopo kwa sasa ni umaliziaji.Mradi huo umegharimu fedha kiasi cha shilingi 136,000,000.00 chanzo cha fedha za mradi huo zinatokana na Ruzuku ya serikali ya miradi ya maendeleo CDG. Mradi huo utakamilika ifikapo Desemba 31 2014.
Mojawapo ya Barabara za Lami zilizopo mjini Masasi
Chumba cha maabara ya kisasa iliyopo kwenye shule ya sekondari ya kutwa ya Marika
Maabara katika shule ya sekondari ya kutwa ya Anna Abdallah
Chumba cha maabara sekondari ya Mpindimbi
WODI ya wazazi iliyopo
katika Hospitali ya Halmashauri ya mji Masasi-Mkomaindo ambayo imejengwa kwa
fedha za kitanzania shilingi 85,000,000 kutokana na fedha za CDG.Ujenzi wa wodi
hiyo ulianza oktoba 01,2013 na kukamilika Julai 8,2014 na kwamba tayari wodi
hiyo kwa sasa inatumika
Nyumba ya mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD