TANGAZO
DIWANI wa kata ya Michiga Hashimu Nassir (Kulia) akikabidhi mabeseni kwa kaimu mkuu wa kituo cha Afya cha Michiga Jofrey Jally ikiwa ni miongoni mwa vifaa alivyovikabidhi hii leo.
Na Clarence Chilumba,
Nanyumbu.
DIWANI
wa kata ya Michiga jimbo la Nanyumbu mkoani Mtwara,Hashimu Nassir (CCM) amenunua vifaa vya kujifungulia akinamama
wajawazito vyenye thamani ya shilingi laki saba ambapo kila mjazito ambaye yupo katika kata
hiyo atahudumiwa bure kwa kutumia vifaa
hivyo pale anapoenda kujifungua.
Vifaa
alivyonunua na kuvikabidhi leo katika kituo cha afya cha Michiga ni pamoja groves
za kuvaa mikokoni,beseni za kuwekea maji,sindano pamoja na nailoni ngumu ambazo mama mjamzito
hutandika wakati anapojiandaa kujifungua.
Pia
diwani huyo amekabidhi vifaa vya mfumo wa umeme jua (Solar) katika kituo hicho
cha afya kwa lengo la kuondoa kero iliyodumu kwa muda wa miaka miwili
iliyowalazimu wajawazito kujifungulia kwa kutumia mwanga wa tochi za simu
nyakati za usiku.
Diwani
huyo ameamua kununua vifaa hivyo kwa fedha zake za mfukoni kwa lengo la
kuwaondolea kero akinamama wajawazito pamoja
na wananchi kwa ujumla wanaopata huduma katika kituo hiko ambapo awali akinamama hao walijifungulia gizani sambamba
na kutakiwa kubeba vifaa vya kujifungulia.
Akizungumza
wakati wa kukabidhi vifaa hivyo,diwani huyo alisema huu ni wakati wa viongozi
wa kisiasa na serikali kutekeleza ahadi walizoziahidi kwa wananchi wakati
wanaomba kuchaguliwa na kwamba ataendelea kufanya hivyo katika kipindi chote
cha uongozi wake.
“Nimeguswa na tatizo la wajawazito
wanapokwenda pale kwenye kituo cha afya nyakati kujifungua gizani huku
wakilazimika kutumia mwanga wa simu na vibatari…mbaya zaidi ni pale
wanapoelezwa kuwa hakuna vifaa vya kujifungulia na kutakiwa
wakanunue wenyewe ndio maana nimeamua kununua kwa ajili ya wajawazito wa kata
yangu”.alisema Nassir.
Alisema
kituo hiko ni muhimu kwa wananchi wengi wa maeneo hayo hata wale wa wilaya
jirani ya Tunduru mkoani Ruvuma ambapo ameiomba serikali ya awamu ya tano
kukiangalia kituo hiko kwa jicho la tatu ili kiweze kutoa huduma bora kwa
wwananchi hao.
Kwa upande wake kaimu mkuu wa
kituo cha afya cha Michiga Jofrey Jally alisema kituo hiko chenye uwezo wa
kuhudumia wagonjwa 90 hadi 100 kwa siku kinakabiliwa na changamoto mbalimbali
ikiwemo ukosefu wa dawa,jumba la wagonjwa,ukosefu wa miundo mbinu rafiki kwa
wagonjwa pamoja na uzio kwa ajili ya usalama.
Alisema kutokana na kituo hiko
kuhudumia wagonjwa wengi kutoka katika vijiji vya Michiga,Pachani,Mnazimmoja
pamoja na Nandembo kumesababisha kuwepo na mlundikano wa wagonjwa na hivyo
kushindwa kutoa huduma kikamilifu.
“Licha ya kituo hiki kuhudumia
wagonjwa kutoka katika vijiji hivyo…pia tunapokea wagonjwa wengine kutoka
katika vijiji vyenye zahanati ambao wameshindwa kuwahudumia na vijiji hivyo ni
Makong’onda,Lumesule,Nakopi,Mburusa na Likokona”alisema Jally.
Kituo cha afya cha
Michiga,kata ya Michiga,Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara ni miongoni
mwa vituo vikubwa wilayani humo huku kikiwa kinakabiliwa na changamoto
mbalimbali.
BAADHI ya watumishi wa kituo cha afya cha Michiga pamoja na wananchi wa kata hiyo wakimsikiliza diwani wa kata hiyo (hayuko pichani) wakati wa kukabidhi vifaa hivyo kwa kitu hiko.
DIWANI wa kata ya Michiga Hashimu Nassir akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo.
BAADHI ya wagonjwa wakiwa wamelala kwenye moja ya wodi iliyofungwa mfumo wa umeme jua vifaa vilivyonunuliwa na diwani wa kata hiyo ya Michiga Hashim Nassir.
MZEE Moizi Nkakia akitoa shukrani kwa niaba ya wananchi wa kata ya Michiga baada ya diwani kukabidhi vifaa hivyo.
KAIMU mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nanyumbu Bwana Ajika akizungumza wakati wa tafrija ya kukabidhi vifaa katika kituo cha afya cha Michiga.
Diwani wa kata ya Michiga na kaimu mwenyekiti wa CCM wilaya ya Nanyumbu Bwana Ajika wakipata maelezo kutoka kwa mganga wa kituo hiko kwenye chumba cha upasuaji katika kituo hiko cha afya.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD