Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

WAZIRI AIPONGEZA HOSPITALI YA MKOMAINDO KWA UKUSANYAJI WA MAPATO KWA MFUMO WA KIELEKTRONIKI.

TANGAZO
 KAIMU mganga mkuu Hospitali ya Mkomaindo Halmashauri ya mji wa Masasi DK. Mussa Rashid akitoa taarifa kwa waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu aliyefanya ziara hii leo hospitalini hapo.

Na Clarence Chilumba,Masasi.
WAZIRI wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu ameupongeza uongozi pamoja na wafanyakazi wote wa hospitali ya Mkomaindo Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara kwa jitihada zake katika ukusanyaji wa mapato kwa kutumia mfumo wa kisasa wa kielektroniki ikiwa ni utekelezaji wa agizo la serikali.

Ukusanyaji wa mapato katika hospitali hiyo umeongezeka kutoka shilingi 500,000 kwa siku kabla ya kufungwa kwa mfumo huo hadi shilingi 1,500,000, kwa siku baada ya  kuanza kutumia mfumo wa ki-elekroniki wa ukusanyaji wa mapato katika Hospitali ya Mkomaindo mjini Masasi.

Pongezi hizo amezitoa hii leo mjini hapa wakati wa ziara yake ya kikazi iliyokuwa na lengo la kukagua shughuli mbalimbali za sekta ya afya pamoja na kusikiliza kero mbalimbali kutoka kwa watumishi wa idara ya afya ambapo alisema kitendo cha kuongezeka kwa mapato katika hospitali hiyo kinapaswa kuigwa.

 BAADHI ya watumishi wa afya na wale wasio wa afya wakimsikiliza kwa makini waziri wa afya Ummy Mwalimu (Hayupo pichani) wakati anaongea nao hii leo nje ya hospitali hiyo baada ya kuwasili kwa ziara yake ya ukaguzi.
 WAZIRI wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akiongea na mmoja wa wagonjwa aliyemkuta hospitalini hapo akiwa anasubiri huduma 

Alisema serikali ya awamu ya tano chini ya Dk.John Pombe Magufuli imejikita zaidi katika ukusanyaji wa mapato kwa lengo na kutoa huduma bora kwa wananchi huku akizitaka Halmashauri zote nchini kuiga mfano wa hospitali ya mkomaindo kwa mafanikio yake katika suala la ukusanyaji wa mapato.

Alisema pia dhamira ya serikali ni kuimarisha nidhamu,uwazi na uwajibikaji kwa watumishi wote wakiweno wa sekta ya afya na kwamba serikali itendelea kukemea vitendo vyote viovu vnavyofanywa na baadhi ya watumsihi wasio na maadili katika utumishi wa umma.

“Natumia hadhara hii kuziagiza halmashauri zote nchini…kuwa na mifumo ya kisasa ya ukusanyaji wa mapato katika hospitali zake,vituo vya afya pamoja na zahanati kwa lengo la kuokoa fedha nyingi zilizokuwa zinaenda mikononi mwa baadhi ya watumishi na kwamba zinapasa kuiga mfano huu wa Mkomaindo”alisema waziri huyo.

 BAADHI ya Wagonjwa waliokuwa nje ya jengo la Maabara wakisubiri kupewa Huduma hii leo katika hospitali ya Mkomaindo halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara.

 WAZIRI wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akizungumza na mama wa mtoto katika wodi ya uzazi katika Hospitali ya Mkomaindo mjini Masasi hii leo.


Aidha ameuagiza uongozi wa hospitali hiyo kuhakikisha kuwa wanayatumia vizuri makusanyo hayo ya ndani huku akisisitiza kuwa asilimia 50 ya mapato hayo yatumike katika ununuzi wa dawa na vifaa tiba ambapo asilimia 50 inayobaki itumike katika shughuli za uendeshaji wa hospitali.

Alisema ni vyema sasa uongozi wa hospitali hiyo uangalie upya namna ya kutoa motisha kwa wafanyakazi wa hospitali hiyo kwa kutumia makusanyo hayo badala ya kukaa na kusubiri ruzuku kutoka serikali kuu kwa lengo la kuboresha ufanisi na utendaji kazi wa watumishi wa hospitali hiyo.

 BAADHI ya wanachuo wa chuo cha Uuguzi na Ukunga Halmashauri ya Mji wa Masasi wakipiga makofi ikiwa ni ishara ya kumpokea waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Ummy Mwalimu (Hayupo Pichani).
 MMOJA wa watumishi wa Hospitali ya Mkomaindo Halmashauri ya mji wa Masasi akitoa maelezo kwa waziri wa afya wakati wa kikao cha waziri huyo na watumishi wa Hospitali ya Mkomaindo mjini Masasi.

“Tumieni makusanyo yenu ya ndani katika kutoa motisha kwa watumishi wa hospitali yenu…viko baadhi ya vitu havihitaji pesa kutoka serikali kuu kama vile malipo ya muda wa ziada na kazi zinginezo mnazoona kuwa mtumishi anapaswa kulipwa kwani kwa kufanya hivo kutasaidia kutatua kero mbalimbali zinazowakabili watumishi”.alisema waziri Ummy.

Katika hatua nyingine waziri huyo ameimwagia sifa hospitali hiyo kwa kufanikiwa kupunguza idadi ya vifo vinavyotokana na uzazi  kutoka vifo  22 mwaka 2014 hadi 12 mwaka 2015 sawa na asilimia 45 kutokana na uhamasishaji na elimu ya afya inayotolewa kwa akina mama na jamii juu ya umuhimu wa kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma za afya.

 WAZIRI wa afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akipata maelezo kutoka kwa wagonjwa hospitalini hapo ambapo wengi walipongeza huduma bora zinazotolewa.

 WAZIRI Ummy Mwalimu wakati wa kikao na watumishi wa Hospitali ya Mkomaindo Mjini Masasi.

 WAZIRI wa Afya Ummy Mwalimu akisaini kitabu cha wageni Hii leo Ikulu wilayani Masasi.

 Wanachuo wa chuo cha Ukunga na Uuguzi pamoja na wananchuo wa chuo cha CATC Vyote vikiwa Halmashauri ya Mji wa Masasi nao pia walipata Fursa ya kuzungumza na Waziri wa afya Ummy Mwalimu.


Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,jinsia,wazee na watoto Ummy Mwalimu akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Mkomaindo Mjini Masasi hii leo.Kulia kwake ni Mkuu wa Wilaya ya Masasi Bernald Nduta na kushoto ni Mganga Mkuu wa serikali Profesa Mohamed Kambi.


WATUMISHI wa Idara ya Afya Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara wakimsikiliza Waziri wa afya,maendeleo ya jamii,jinsia,wazee na watoto wakati wa kikao chake na watumishi hao hii leo mjini Masasi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top