TANGAZO
PAROKO wa Kanisa Katoliki Parokia ya Masasi Jimbo la Tunduru Masasi Dominick Mkapa(Picha ya Maktaba).
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
Paroko wa
kanisa katoliki parokia ya Masasi jimbo la Tunduru Masasi, mkoani Mtwara, Dominick
Mkapa amewataka viongozi waliopewa dhamana katika idara ya mahakama nchini kutenda haki katika kutoa hukumu ili kuonesha tofauti
na hukumu yenye "utata" ya kifo iliyotolewa na Pilato kwa Yesu Kristo.
Ameyasema hayo
leo mjini hapa wakati wa ibada ya ijumaa kuu iliyofanyika katika kanisa
katoliki parokia ya Masasi,ambapo amesema hukumu ya kifo iliyotolewa na Pilato wakati huo ilijaa utata
na uongo mazingira yaliyopelekea Yesu Kristo kuuawa kwa makosa ambayo
kiuhalisia hakuyatenda.
Ijumaa Kuu ni siku ambayo wakristo nchini
huungana na wakristo wenzao Duniani kote kwa kuadhimisha mateso ya Yesu Kristo
Msalabani siku ambayo wanaitumia kama siku ya kumbukumbu ya mateso na kufa kwa
mwokozi wao Bwana Yesu Kristo ambaye aliletwa na Mungu ili kuja kuukomboa
ulimwengu uliojaa dhambi.
Amesema
kushindwa kwa Pilato kusimama katika haki,woga pamoja na shinikizo kutoka kwa
Wayahudi ndizo baadhi ya sababu zilizopelekea Yesu Kristo kuhukumiwa kusulubiwa
msalabani na hatimaye kifo huku akikiri kuwa sababu kama hizo hutumika hata
sasa katika baadhi ya hukumu.
Amesema
kimsingi hata makosa ambayo Bwana yesu kristo alishitakiwa nayo hayana ukweli
wowote ambapo alionesha wazi kusikitishwa na uamuzi wa Pilato wa kutoa hukumu
kubwa kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa Wayahudi.
“Natumia ibada
hii ya ijumaa kuu kutoa wito kwa mahakama nchini…zitoe adhabu katika misingi ya
haki na usawa na bila ya shinikizo kutoka kwa mtu yeyote ili kuepuka kutoa
hukumu zenye utata na uonevu kama ile aliyopewa bwana yesu kristo na Pilato”.alisema
Mkapa.
Amesema hata
sasa nchini kumekuwa na baadhi ya hukumu zenye utata kama iliyotolewa na Pilato
huku akiwataka waliopewa dhamana katika kutoa maamuzi mbalimbali kuzingatia
kanuni na sheria za nchi bila upendeleo wowote.
“Hukumu
iliyotolewa na Pilato wakati wa utawala wa Warumi chini ya mfalme Kaisar…haina
tofauti na baadhi ya hukumu zinazotolewa hivi sasa katika baadhi ya mahakama
nchini hivyo ni vyema wanaokutwa na makosa wakatendewa haki”alisema Mkapa.
Kwa mujibu
wa Mkapa alisema mateso ya Bwana Yesu Kristo yaliyopelekea kifo chake yawe
fundisho kwa watanzania ambapo wanapaswa kuishi kwa amani na upendo kama
inavyompendeza mungu.
Katika ibada
hiyo ya ijumaa kuu waumini wa kanisa katoliki parokia ya Masasi walipata fursa
pia ya kubusu msalaba ikiwa ni kielelezo,mfano
na taswira ya kufundisha kwa lengo la kujua kwa urahisi jinsi ile mkombozi wao
alivyotundikwa juu ya mti ule wa msalaba.
Aidha ibada hiyo ilihudhuriwa na Rais mstaafu
wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa ambaye yuko mjini Masasi kwa mapumziko ya
sikukuu ya ufufuko wa bwana yesu Kristo (Pasaka).
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD