TANGAZO
Wanachama wa CCM wakishangilia ushindi baada ya kutangazwa kwa matokeo ya diwani wa kata ya Mkomaindo jimbo la Masasi Salvatory Salumu Ally hii leo.
Na Clarence Chilumba,Nanyumbu.
Mgombea ubunge jimbo la Nanyumbu mkoani Mtwara kupitia chama cha
Mapinduzi (CCM) Dua William Mkurua ameibuka kidedea kwa kupata ushindi wa
kishindo na kuwagaragaza wapinzani wake wa chama cha CUF na Chadema.
Akitangaza matokeo hayo hii leo msimamizi wa uchaguzi jimbo la Nanyumbu
Idris Mtandi alisema katika uchaguzi huo jumla ya wananchi 82,398 walijitokeza
katika zoezi la kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura huku watu
59,431 walipiga kura ambapo kura haalali ni 57424 na kura 2007 zikiharibika.
Alisema Dua William Mkurua wa chama cha mapinduzi alipata kura 36,175
sawa na asilimia 63, Majaribu Hassan Lupeto wa chama cha wananchi CUF alipata
kura 13,067 sawa na asilimia 23 huku Nyuchi Mansa Alfred wa chama cha
demokrasia na maendeleo Chadema akiambulia kura 8182 sawa na asilimia 14.
Akizungumzia kuhusu matokeo ya udiwani katika jimbo hilo Idris alisema
jumla ya kata 17 zilishiriki uchaguzi huo ambapo chama cha mapinduzi
kimejizolea ushindi kwa kupata viti 15,chadema ikipata kiti kimoja na CUF nayo
ikiambulia kiti kimoja.
Aidha katika uchaguzi huo Chama cha mapinduzi kimefanikiwa kurejesha
kiti chake kimoja cha udiwani katika kata ya Lumesule iliyokuwa ngome ya CUF
kwa kipindi kirefu.
Akizungumzia kuhusu namna uchaguzi huo ulivyokuwa alisema uchaguzi
umefanyika kwa amani na utulivu ambapo wananchi wengi hususani vijana walijitokeza
kupiga kura kwenye uchaguzi huo.
Katika hatua nyingine chama cha mapinduzi jimbo la Ndanda wilayani
Masasi kimepoteza jimbo hilo kwa mgombea wake Mariam Kasembe kupata kura 26,215
na kupoteza jimbo hilo jipya.
Akitangaza matokeo hayo msimamizi wa uchaguzi jimbo la Ndanda Beatrice
Dominick alimtangaza Cesil David Mwambe wa chama cha demokrasia na maendeleo
chadema kuwa mshindi aliyepata kura 26,247.
Wagombea wengine ni Angelus Thomas Millanzi wa chama cha NLD alipata
kura 447 na Edward Millanzi wa chama cha ACT-Wazalendo alipata kura 923.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD