TANGAZO
Na
Clarence Chilumba,Nanyumbu
WATU
zaidi ya 7948 wilayani Nanyumbu mkoani Mtwara wamenufaika na mpango wa kunusuru
kaya masikini unaotekelezwa na mfuko wa
maendeleo ya jamii (TASAF III)wilayani humo kwa kupatiwa ruzuku ya
sh.231,365,636.36 milioni na kwamba hatua hiyo imewawezesha kubadili hali ya
maisha ndani ya familia zao.
Hayo
yalisemwa mwishoni mwa wiki na mratibu wa TASAF wilaya ya Nanyumbu Rajabu
Kilozo wakati anazungumza na baadhi ya
kaya za vijiji vya Sengenya pamoja na Masialele vilivyopo wilayani humo wakati
wa mwendelezo wa uhawilishaji rasilimali fedha kwa kaya hizo ambapo timu ya
Halmashauri iliongozana kwa ajili kwenda kujionea jinsi ya ugawaji wa ruzuku
unavyofanyika kwa walengwa.
Alisema
wameamua kufanya ziara kwa kuwashirikisha viongozi mbalimbali wa Halmashauri
akiwemo mkurugenzi mtendaji,Ally Kasinge pamoja na ofisi ya mkuu wa wilaya hiyo
kwa ajili ya kwenda kujionea jinsi zoezi la uhawilishaji wa ruzuku
unavyofanyika kwa walengwa ili nao waweze kutoa mchango wao wa mawazo katika
mpango huo wa kunusuru kaya masikini.
Alisema kuna aina nne za ruzuku zinazotolewa kwa kaya
zilizoandikishwa kwenye mpango huo wa kunusuru kaya masikini na kwamba aina
hizo ni ruzuku ya msingi bila masharti yoyote,ruzuku ya kutimiza masharti
kuhudhuria kliniki na shuleni kwa kaya yenye watoto pamoja na mama mjamzito.
Kilozo
alizitaja aina ya ruzuku zingine zinazotolewa kuwa ni ujira kwa mwanakaya mmoja
kutoka kaya zilizoandikishwa ambaye atashiriki katika kazi za ujenzi na
kuboresha miundombinu pamoja na hifadhi ya mazingira na ruzuku nyingine ni
ruzuku ya kutimiza masharti ya kuhudhuria shuleni kwa wanafunzi wanaosoma
kidato cha kwanza hadi cha sita.
Mratibu
huyo alieleza kuwa Halmashauri ya Nanyumbu kupitia mfuko wa maendeleo ya jamii TASAF
imefuata taratibu zote kwa kuhusisha viongozi wa kijiji,mtaa kwa kufanya
mikutano ya hadhara ili kuweka na kukubaliana vigezo vya umasikini katika eneo
husika kwa kuongozwa na wataalamu wa TASAF wilayani humo.
“kwa
upande wetu hadi sasa zoezi la uhawilishaji rasilimali fedha kwa walengwa
umefanyika vizuri na hakuna malalamiko yoyote yaliyojitokea kutoka kwa walengwa
wa mpango huu hivyo ndio maana tumekuja timu mzima ya Halmashauri ili wajonee
wenyewe”.alisema Kilozo.
Kwa
upande wake somoe lini (54) ambaye alipatiwa ruzuku ya sh. 40,000 ni mkazi wa
kijiji cha Masialele alisema kuwa mpango huo umemnufaisha kwa kuweza kupata bati
na kupauwa nyumba yake ambayo ilikuwa haijapauliwa kwa kokosa fedha pia ameweza
kununua kuku kwa ajili ya kuanza ufugaji
Nae
Sesilia Msonela ambaye ni mkazi wa kijii cha Masielele alipatiwa ruzuku ya sh.30,000 alisema kuwa ameweze kununua
pembejeo za kilimo na kulima ambapo kupitia mazao aliyopata ameweza kununua
chakula kwa ajili ya familia yake na ameomba mpango huo uendelee kuziangalia
kaya masikini ili kuziinua kiuchumi kama unavyofanyika kwa sasa.
Mwisho
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD