TANGAZO
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
Wakazi
watano wa wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wamepandishwa kizimbani kujibu shitaka
linalowakabili la kujihusisha na huhujumu uchumi wa nyara za serikali ikiwemo usafirishaji wa meno
ya tembo kutoka wilayani masasi kuelekea
mikoa ya jirani nchini.
Watuhumiwa
waliofikishwa mahakamani hapo jana jumatano kujibu shitaka hilo ni Bosco Simoni Mwehinda
(37) mkazi wa mtaa wa Jida,Daniel Nyangimolet (29) mkazi wa Matankini, Salumu
Abdulrahamani (37) mkazi wa mtaa wa Mtandi Said Halifa (43) mkazi wa Wapiwapi
pamoja na Msafiri Emanuel Mapuga (37) mkazi wa Matankini Hassani wote wakiwa ni
wakazi wa mji wa Masasi.
Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama ya
wilaya ya Masasi Asha Mwetindwa mwendesha mashtaka ambaye ni mwanasheria
mwandamizi wa serikali Mwahija Ahmad alidai kuwa watuhumiwa hao wanashukiwa
kujihusisha na vitendo vya usafirishaji wa meno ya tembo kwa kipindi cha muda
mrefu sasa.
Ahmad
alidai kuwa watuhumiwa hao walitenda makosa hayo ya ujangili kwa vipindi
tofauti mwanzoni mwa mwaka jana katika maeneo mbalimbali wilayani humo huku
wakijua kuwa ni kosa la jinai kufanya vitendo hivyo vya kuhujumu uchumi wa
nchi.
Alidai
kuwa watuhumiwa hao hawakutakiwa kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina
mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo na kwamba kwa sasa iko kwenye hatua za awali za
uchunguzi na uchunguzi huo utakapokamilika kesi hiyo itahamishiwa mahakama ya
mkoa Mtwara.
Watuhumiwa
hao wako nje kwa dhamana inayowataka
kuwa na mwenendo na tabia njema ndani ya
kipindi cha miaka mitatu (03) ambapo wanatakiwa kuripoti mahakamani kila
jumatatu ya mwanzo wa mwezi huku
wakitakiwa kutojihusisha na vitendo vyovyote vya kihalifu katika kipindi hicho
chote.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD