Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

#Mama Janeth Magufuli Amwaga Neema Ya Chakula Kwa Wazee Wa Kambi Ya Kijiji Cha #Nkaseka Wilayani Masasi.

TANGAZO
 MKE wa Rais Mama Janeth Magufuli akimkabidhi mmoja wa wazee waliopo katika kambi 
ya wagonjwa wa ukoma katika kijiji cha Nkaseka wilayani Masasi.

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli amemshukuru Mtumishi wa Mungu wa Kanisa la SCOAN la Nchini Nigeria Nabii TB Joshua kwa kutambua jitihada zake za kusaidia Wazee, Walemavu na watu wasiojiweza.
Shukrani hizo amezitoa wakati akikabidhi msaada wa Vyakula, Mavazi, Dawa na Vifaa vya Malazi katika kituo cha Nkaseka kilichopo Wilayani Msasi Mkoani Mtwara.
Aidha Mama Janeth Magufuli alitoa rai kwa wasimamizi wa vituo vya kulea Wazee, walemavu na watu wasiojiweza kuwa waaminifu na kuacha tabia ya kuuza vitu vya Msaada vinavyotolewa na wadau mbalimbali kwa ajili ya kundi hilo kwani bado linauhitaji mkubwa.
Naye Mke wa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Mary Majaliwa aliwaomba wadau wengine kujitokeza na kuunga mkono jitihada hizo za kusaidia makundi ya watu wenye mahitaji Maalum.
Mama Magufuli ataendelea na Ziara yake kesho katika Mkoa Lindi kwa Kutembelea Kambi ya Wazee ya NANDANGA iliyopo Ruangwa Mkoani humo.


 Mama Janeth Magufuli akiwa na viongozi wa chama na serikali,kushoto kwake ni mke wa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Majaliwa na mkuu wa wilaya ya Masasi Mh: Bernald Nduta. Kulia kwake ni mkuu wa mkoa wa Mtwara Mh: Halima Dendego na mwenyekiti wa CCM mkoa wa Mtwara Mh;Sinani.

Mke wa Rais mama Janeth Magufuli akisalimiana na bibi kizee katika kambi hiyo ya wagonjwa wa ukoma.

 Mama Magufuli akipokea zawadi kutoka kwa wazee hao 

 Mkuu wa wilaya ya Masasi Mh: Bernald Nduta akisalimiana na mke wa Rais mama Janeth Magufuli.
 Wazee wanaoishi katika kambi ya wagonjwa wa ukoma katika kijiji cha Nkaseka wilayani Masasi.

 Mama Janeth Magufuli akiwahutubia wazee na wananchi waliojitokeza kumsikiliza.

 Mmoja wa bibi kizee akitoa neno la shukrani kwa mke wa Rais mama Janeth Magufuli pamoja na mke wa waziri mkuu.
 Mke wa waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mama Majaliwa akizungumza na wananchi wa kijiji cha Nkaseka wilayani Masasi.

 Mama  Janeth Magufuli akitia saini kitabu cha wageni.

 Mama Janeth Magufuli akiteta jambo na mke wa waziri mkuu mama Majaliwa.
MKUU wa mkoa wa Mtwara Mh:Halima Dendego akizungumza na wananchi pamoja na wazee wa kambi ya Nkaseka wilayani Masasi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top