Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

#Halmashauri Ya Mji Masasi #Yakamilisha Utengenezaji Wa Madawati Kwa Asilimia 80 Kwa Shule za Msingi na Sekondari.

TANGAZO
 BAADHI ya maeneo ya utengenezaji wa Madawati katika kituo cha Wapiwapi mjini Masasi.

Na Clarence Chilumba,Masasi.
HALMASHAURI ya mji wa Masasi mkoani Mtwara imefanikiwa kukamilisha utengenezaji wa Madawati kwa shule za msingi na sekondari  kwa asilimia 80 hadi sasa huku jitihada zingine za kukamilisha zoezi hilo ifikapo Juni 30, 2016 zikiwa zinaendelea.

Hadi sasa jumla ya madawati 1446 tayari yameshatengenezwa kati ya madawati 2329 yaliyohitajika  kwa shule 32 za msingi za Halmashauri hiyo ambapo madawati 883 yaliyobakia tayari mbao zimeshapatikana huku utengenezaji wa madawati hayo ukiwa mbioni kukamilika mwishoni mwa wiki hii.

Akizungumza kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi Geofrery Martin alisema kwa sasa ili kukamilisha kwa wakati zoezi hilo wameweka vituo vitano vya utengenezaji wa madawati hayo ambavyo ni pamoja na Nyasa,Wapiwapi,Mkuti,Wabiso pamoja na Kisiwani.

Alisema katika vituo hivyo vitano kituo cha Nyasa kinatarajia kutengeneza jumla ya madawati 224 ambapo kati ya hayo 73 ni kwa ajili ya shule ya msingi Maendeleo na 151 ni kwa ajili ya shule ya msingi Nyasa na kituo cha Wapiwapi kitatengeneza madawati 177 kwa ajili ya shule ya msingi Kambarage.

Aidha katika kituo cha Mkuti kinatarajia kutengeneza madawati 166 kwa ajili ya shule ya msingi Mkuti,Kituo cha Kisiwani Madawati 166 kwa ajili ya shule ya msingi Sabasaba na katika kituo cha Wabiso kitatengeneza madawati 152 kwa ajili ya shule ya msingi Mkomaindo.

“Tuko katika hatua nzuri ya umaliziaji wa zoezi la utengenezaji wa madawati kwa shule zetu za msingi…kwa sasa tulichofanya ni kugawa kazi katika vituo mbalimbali vya utengenezaji na tunaamini ifikapo jumapili wiki hii tutakuwa tumekamilisha zoezi hili”.Alisema Martin.

Alisema Kutokana na kuwepo kwa mpango wa elimu bila malipo  wazazi mjini humo walijitokeza  kwa wingi kupeleka watoto wao shuleni  mazingira ambayo yalisababisha kuwepo kwa idadi kubwa ya wanafunzi kwenye shule za msingi ambapo jumla ya wanafunzi 20,957 waliandikishwa kuanza darasa la kwanza.

Alisema kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi kuandikishwa kwenye shule zote zilizopo katika Halmashauri hiyo kumekuwa na changamoto kubwa kwa baadhi ya shule hizo kwa wanafunzi wake kukaa chini kutokana na upungufu wa madawati.

Katika hatua nyingine kaimu mkurugenzi huyo wa Halmashauri ya mji wa Masasi alisema tayari zoezi la utengenezaji wa viti pamoja na meza 778 kwa shule 10 za sekondari za halmashauri hiyo umekamilika na tayari wameshasambaza mashuleni.




Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara Mheshimiwa Sospeter Nachunga (Kushoto) akisikiliza maelezo kutoka kwa Fundi anayetengeneza Madawati hayo katika kituo cha Wapiwapi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top