Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

#Timu Ya Soka Ya Halmashauri Ya Mji Wa #Masasi Yapoteza Mechi Yake Ya Kirafiki Dhidi Ya #JWTZ Kambi Ya Masasi.

TANGAZO

Na Clarence Chilumba,Masasi TC.
TIMU ya soka ya Halmashauri ya Mji wa Masasi (MASASI TC FC) kwa mara nyingine tena imeshindwa kuibuka kidedea katika mechi zake za kirafiki ambazo timu hiyo imekuwa ikicheza kwa siku za hivi karibuni lengo likiwa ni kudumisha amani,kuburudisha pamoja na kudumisha undugu baina yao na taasisi nyingine zilizopo mjini humo.

Katika mechi iliyochezwa leo katika uwanja wa Boma mjini Masasi,Timu hiyo ilijikuta ikiambulia kichapo kutoka kwa Vijana wa JWTZ Kambi ya Masasi ambao walifanikiwa kuifunga Masasi FC magoli matatu (3) kwa sifuri (0).

Mechi hiyo iliyoshuhudiwa na mashabiki Lukuki ilianza kwa kasi huku kila timu ikijaribu kupata bao la kuongoza lakini hali haikuwa hivyo mara baada ya timu zote kumaliza kipindi cha kwanza zikiwa hazijafungana.

Kipindi cha pili timu zote zilifanya mabadiliko kadhaa lakini mabadiliko hayo yalionekana kuwabeba zaidi timu ya JWTZ ambayo ilifanikiwa kupata bao kunako dakika ya 50 ya kipindi hiko cha pili na kuwafanya wapinzani wao Masasi TC FC kupigana katika kutafuta bao la kusawazisha.

Licha ya wachezaji wa Masasi TC kucheza kwa “JIHADI” kutafuta bao la kusawazisha na bao la kuongoza hali ilikuwa tofauti baada ya JWTZ kujipatia mabao mawili ya harakaharaka na kufanikiwa kuongoza kwa jumla ya magoli matatu bila majibu kutoka kwa wapinzani wao.

Mechi hiyo iliyokuwa kali na ya kusisimua iliisha kwa JWTZ kambi ya Masasi kupata ushindi wa mabao matatu kwa sifuri na kuifanya Timu ya Masasi TC kupoteza mechi ya Pili mfululizo kwani katika mechi iliyopita walifungwa kwa Tabu na Masasi Veterans.

  KIKOSI cha Timu ya Halmashauri ya Mji wa Masasi

 KIKOSI cha Timu ya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) Kambi ya Masasi.
 BAADHI ya wapenzi na mashabiki wa Timu ya Halmashauri ya Mji wa Masasi wakifuatilia Mechi.





 WACHEZAJI wa Timu ya Masasi TC wakiwa katika  mapumziko


TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top