Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

Neema Yaja Ruangwa-Barabara ya Lami Kutoka Nanganga-Nachingwea-Ruangwa Kuanza Kujengwa.

TANGAZO
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwahutubia wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Namahema-Ruangwa.

Na Mwandishi Wetu,Ruangwa.
WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa, amesema Serikali inatarajia kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Nanganga, Ruangwa hadi Nachingwea. Hatua hiyo itawezesha kutatuliwa kwa kero ya barabara inayowakabili wananchi wa wilaya za Ruangwa na Nachingwea kwa muda mrefu.
Majaliwa amesema barabara hiyo ambayo kwa sasa haipo katika hali nzuri itajengwa kwa kiwango cha lami. Serikali inatarajia kuanza kuifanyia upembuzi yakinifu katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.
Aliyasema hayo juzi alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Likunja, Nkowe na Namahema katika mikutano ya hadhara aliyoifanya wilayani Ruangwa wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi.
Alisema serikali imejipanga katika kuboresha miundombinu ya barabara kwenye maeneo mbalimbali nchini na kwamba mara baada ya kumalizika kwa upembuzi yakinifu, ujenzi wa barabara hiyo utaanza, hivyo amewataka wananchi kuwa na subira.
Katika hatua nyingine, Majaliwa amewataka wananchi wa vijiji hivyo kushirikiana katika shughuli za maendeleo na kuweka kando itikadi zao za kisiasa kwa sababu uchaguzi ulishamalizika tangu Oktoba 25 mwaka jana.
“Mimi nitaendelea kuwaheshimu, kuwasikiliza na kuwahudumia, nawaomba tushirikiane na tuweke kando masuala ya itikadi za vyama, sasa ni wakati wa kazi, hivyo ni bora tukashirikiana kufanya kazi kwa maendeleo ya Ruangwa jambo ambalo linawezekana.
Hata kama wewe ambaye najua ulinichukia, mimi nimekusamehe kutoka moyoni, wewe ni wangu hata kama hukunichagua nitakuhudumia na kukutumikia kwa sababu mimi ndiye mbunge wako hivyo naomba tushirikiane,” alisema Majaliwa.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Rashid Nakumbya aliomba wakazi wa wilaya hiyo kushirikiana kwa pamoja kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya wilaya yao iweze kupiga hatua.



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitembelea Soko Kuu la Wilaya ya Ruangwa kukagua hali ya upatikanaji na bei za vyakula akiwa katika ziara ya jimbo hilo mkoa wa Lindi jana. (Picha na Ofisi ya waziri mkuu)
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top