Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

Mheshimiwa Majaliwa Aishukia Bodi ya Korosho,Vyama Vya Ushirika...Awaambia Mwisho Wao Umefika.

TANGAZO

Na Bashiru Kauchumbe,Ruangwa.

Serikali imesema ipo mbioni kuufanyia marekebisho mfumo wa ununuzi wa zao la korosho maarufu mfumo wa stakabadhi ghalani  ili wananchi waweze kunufaika na matunda yatokanayo na zao hilo muhimu kwa uchumi wa nchi.

Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Kasimu Majaliwa ambaye yuko wilayani Ruangwa katika mkoa wa Lindi kwa Ziara ya Kikazi aliyoianza hii leo wilayani humo. .

Alisema kuwa mfumo wa Stakabadhi ghalani  umekuwa ukiwanyonya wakulima wa zao la Korosho kutokana na utendaji mbovu wa watendaji wanaosimamia mfumo huo kuanzia vyama vya msingi ,Vyama vikuu vya ushirika na Bodi ya Korosho nchini mazingira yanayosababisha wakulima wa zao hilo kubaki maskini.

Alisema  katika kulitafutia ufumbuzi suala hilo amekutana na Viongozi wa Bodi ya Korosho mapema mwaka huu ili kuondoa baadhi ya vipengele ambavyo vinaonekana kuwanyonya na kuwakandamiza  wakulima wa zao la Korosho nchini.

Alivitaja vipengele hivyo kuwa ni pamoja  na ushuru wa asilimia moja unaokwenda  kwa afisa Ushirika wa Mkoa,Ushuru wa kusafirisha korosho kwenda kwenye maghala ambao ni shilingi 50 kwa kila kilo moja,makato ya shilingi  50 ya chama kikuu cha ushirika,pamoja na riba ya Mkopo wa Benki baada ya chama kupata Mkopo kutoka  Benki.

Kwa mujibu wa Waziri Mkuu amesema kuwa hakuna haja ya kumbebesha Mkulima kulipa gharama hizo kwani kuna baadhi ya vyama vinatumia magari ya vyama kusafirishia korosho mpaka kwenye maghala makuu lakini mzigo wa kulipa gharama hizo anabebeshwa Mkulima huku akiwahakikishia wananchi wilayani Ruangwa kuwa kero hizo zitakwisha.

Akizungumzia kuhusu riba ya Mikopo ya Benki kwa vyama vya msingi alisema sio  lazima gharama hizo kufanywa na Mkulima kwani wanaohusika kufanya  Mikataba ya Mikopo hiyo ni Vyama vya msingi na sio wakulima hivyo vyama vina wajibu wa  kulipa gharama hizo.
 

Kwa upande wa gharama za kulipia maghala makuu  amevitaka vyama vya msingi vilipe vyenyewe gharama hizo au vyama vikuu viende katika maghala ya Vyama vya msingi kwenda kununua Korosho kwa wakulima.

Zao la Korosho nchini Tanzania ni miongoni mwa zao ambalo linaongeza uchumi wa nchi ,lakini tangu kuanzishwa kwa mfumo wa Stakabadhi ghalani katika Mikoa ya Lindi na Mtwara wakulima wengi wa zao hilo wamekuwa wakilalamikia mfumo huo kutokana kuwa na makato yasiyokuwa na tija kwa wakulima ,pamoja na malipo yasiyokuwa na uhakika.

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Lindi Godfrey Zambi ambaye ameambatana na Waziri Mkuu katika ziara hiyo amewataka wakulima wa zao la Korosho Mkoani Lindi kufanya palizi ya Mashamba yao mapema ili kuepusha mikorosho hiyo kuungua moto  nyakati za Kiangazi.




TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top