Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

Wanufaika Wa Mpango Wa Kunusuru Kaya Maskini Nachingwea Waipongeza Serikali Kwa Kuleta Mpango Huo.

TANGAZO


 Christopher Lilai,Nachingwea.
Wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini wilayani Nachingwea, mkoani Lindi wamekiri kuwa mpango huo umekuwa mkombozi mkubwa kwao kwani umeweza kuwabadilisha kimaisha na kuiomba serikali kuongeza kiwango cha ruzuku ili kilingane na thamani halisi ya fedha kwa sasa.
Wakizungumza kwa jana nyakati tofauti na timu ya waandishi wa habari waliotembelea baadhi ya wanufaika hao walisema kiwango kinachotolewa ni kidogo sana ambacho pia kinatolewa kila baada ya miezi mitatu hivyo  serikali ione uwezekano wa kuongeza kiwango hicho na kutolewa kila mwezi.
Samson Nachuruchonga ambaye ni mlemavu wa viungo wa kijiji cha Ntila alisema licha ya kiwango wanachopata kuwa kidogo kimeweza kuwasaidia kugharamia mahitaji muhimu ikiwemo chakula,kusomesha watoto wake kwa kuwanunulia sare na vifaa vya shuleni.
Alisema pia anazitumia fedha hizo kwa kilimo kwani kwa sasa anaweka watu shambani na kuwalipa hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara na kutumia fedha zinazopatikana kupitia kilimo kujijengea nyumba ya bati.
Naye Zainabu Mpunga (73) mkazi wa kijiji cha Chiganga ambaye licha ya kuwa mjane pia anatunza wajukuu wake wawili ambao ni watoto wa marehemu binti yake alisema kuwa ameanza ujenzi wa nyumba kwa kununua bati moja moja kila anapopata ruzuku hiyo na kuwa anatarajia mwaka huu anaratajia kuanzisha ujenzi huo.
Kwa upande wake mratibu msaidizi wa TASAF wilayani Nachingwea,mkoani Lindi, James Mbakile, alisema kuwa kutokana na mpango huo baadhi ya wanufaika wameweza kubadilisha maisha yao kwa kujianzishia miradi midogo midogo ikiwemo ufugaji wa kuku wa kienyeji, nguruwe na mbuzi na kujijengea nyumba za kisasa.
Alisema kuwa jumla ya shilingi Bilioni 2.3 zimenufaisha   kaya 5,850 katika vijiji 69 vya wilayani Nachingwea kupitia mpango wa kunusuru kaya maskini tangu kuanza mpango huo ambao wanufaika wake ni kaya za wazee wasiojiweza na wale wanye magonjwa sugu wamekuwa wakishauriwa kutumia fedha hizo chache kwa kujitafutia chakula,kugharamia masomo na matibabu.
Aidha Afisa mshauri wa kitaalamu wa TASAF wa wilaya hiyo, Dorothy Shiyo aliwaomba viongozi wa serikali za vijiji wawe wasimamizi wa karibu kwa kuwasimamia wananchi kutumia fedha wanazozipata kwa manufahaa ikiwa ni pamoja na kujiwekea akiba.
“Serikali za vijiji viweke washauri wa kwanza katika matumizi  sahihi ya fedha zinazotolewa hivi sasa”alisema Shiyo.

Shiyo aliwaomba walengwa wa mpango huu katika kipindi hiki ambapo kaya nyingi zinakabiliwa na tatizo la chakula kutimia fedha hizo kujinunulia chakula.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top