Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

MAOFISA WA MISITU MKOA WA LINDI WATAHADHARISHWA DHIDI YA UHARIBIFU MKUBWA WA MISITU

TANGAZO
Baadhi ya Vipande Vya mbao vilivyokamatwa na maofisa misitu (Picha ya Maktaba)

Christopher Lilai,Nachingwea.
Mkuu mpya wa mkoa wa Lindi,Godfrey Zambi amewatahadharisha maafisa misitu ambao wilaya zao zitakuwa na uharibifu mkubwa wa  misitu mkoani humo kuwa watakuwa ndio wa kwanza kuchukuliwa hatua kali kwa kushindwa kusimamia misitu.
Akihutubia wananchi wa kijiji cha Lipuyu, wilayani Nachingwea, mkoani Lindi wakati wa siku ya upandaji miti kimkoa iliyofanyika katika kijijini hapo siku ya jumanne, ambapo pia alizindua mradi wa maji katika kijiji hicho alisema haiwezekani uharibifu mkubwa wa misitu uendelee kuwepo wakati wapo wanaotakiwa kusimamia kwa kudhibiti vitendo hivyo.
Alisema kuwa baadhi ya maafisa misitu ndio chanzo kikubwa cha ukataji miti ovyo kwani ndio wanaoruhusu mazao ya misitu kusafirishwa bila ya kuzingatia taratibu na sheria zinazosimamia misitu.
Aidha Mkuu huyo wa mkoa ambaye ameteuliwa hivi karibuni na Rais John Magufuli aliwataka wananchi mkoani hapa kutofanya shughuli za kibinadamu zinazoathiri misitu hasa kilimo cha ufuta kwani madhara ya ukataji wa miti hayawezi kuonekana   kwa haraka bali vizazi vijavyo ndio watakaopata athari zaidi.
“Kama wazee wetu wangemaliza misitu yote leo hii hali ingekuwaje na kama kilimo yapo maeneo ambayo yameruhusiwa kwa shughuli za kibinadamu hivyo wananchi wafuate taratibu za zilizowekwa katika maeneo yao”alisema Zambi.
Katika hatua nyingine Mkuu huyo wa mkoa  ambaye aliyefanya ziara yake ya kwanza mara baada ya kuapishwa wiki iliyopita aliwataka wakuu wa wilaya na wakurugenzi watendaji  mkoani Lindi kuhakikisha  wanafanya ukaguzi wa mara kwa mara kuhakikisha kuwa idadi ya miti inayopandwa kila mwaka inafikia milioni moja na nusu kama lengo lililowekwa kitaifa na pia kama bado inaendelea  kutunzwa.
Alisema haiwezekani  kila mwaka kumekuwa na siku ya upandaji miti lakini hakuna anayehakiki kama idadi inayopandwa inafikia au miti hiyo inaendeleaje kutunzwa hadi sasa.
Aliwataka viongozi hao kuwa na ratiba ya kufanya ukaguzi wa maeneo yaliyopandwa miti wiki mbili kabla ya siku ya upandaji wa miti kwenye maeneo yao ili kujiridhisha kama miti iliyopandwa mwaka uliopita kama ipo kuliko kupanda miti kila mwaka huku inayopandwa haitunzwi.

“Haiwezekani kila mwaka inapandwa miti lakini hatuna uhakika kama inaendelea kuwapo na tena kila mwaka idadi miti inayopandwa inatakiwa kuwa milioni moja na nusu je inafikia idadi hiyo”alihoji Zambi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top