Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

Paroko Wa Kanisa Katoliki Masasi: Hukumu Ya Pilato Kwa Bwana Yesu Kristo Ilijaa Utata,Uonevu na Shinikizo

TANGAZO
PAROKO wa Kanisa Katoliki Parokia ya Masasi Jimbo la Tunduru Masasi Dominick Mkapa(Picha ya Maktaba).

Na Clarence Chilumba,Masasi.
Paroko wa kanisa katoliki parokia ya Masasi jimbo la Tunduru Masasi, mkoani Mtwara, Dominick Mkapa amewataka viongozi waliopewa dhamana katika idara ya mahakama nchini  kutenda haki katika kutoa hukumu ili kuonesha tofauti na hukumu yenye "utata" ya kifo iliyotolewa na Pilato kwa Yesu Kristo.

Ameyasema hayo leo mjini hapa wakati wa ibada ya ijumaa kuu iliyofanyika katika kanisa katoliki parokia ya Masasi,ambapo amesema hukumu ya kifo  iliyotolewa na Pilato wakati huo ilijaa utata na uongo mazingira yaliyopelekea Yesu Kristo kuuawa kwa makosa ambayo kiuhalisia hakuyatenda.

Ijumaa Kuu ni siku ambayo wakristo nchini huungana na wakristo wenzao Duniani kote kwa kuadhimisha mateso ya Yesu Kristo Msalabani siku ambayo wanaitumia kama siku ya kumbukumbu ya mateso na kufa kwa mwokozi wao Bwana Yesu Kristo ambaye aliletwa na Mungu ili kuja kuukomboa ulimwengu uliojaa dhambi.

Amesema kushindwa kwa Pilato kusimama katika haki,woga pamoja na shinikizo kutoka kwa Wayahudi ndizo baadhi ya sababu zilizopelekea Yesu Kristo kuhukumiwa kusulubiwa msalabani na hatimaye kifo huku akikiri kuwa sababu kama hizo hutumika hata sasa katika baadhi ya hukumu.

Amesema kimsingi hata makosa ambayo Bwana yesu kristo alishitakiwa nayo hayana ukweli wowote ambapo alionesha wazi kusikitishwa na uamuzi wa Pilato wa kutoa hukumu kubwa kwa sababu ya shinikizo kutoka kwa Wayahudi.

“Natumia ibada hii ya ijumaa kuu kutoa wito kwa mahakama nchini…zitoe adhabu katika misingi ya haki na usawa na bila ya shinikizo kutoka kwa mtu yeyote ili kuepuka kutoa hukumu zenye utata na uonevu kama ile aliyopewa bwana yesu kristo na Pilato”.alisema Mkapa.

Amesema hata sasa nchini kumekuwa na baadhi ya hukumu zenye utata kama iliyotolewa na Pilato huku akiwataka waliopewa dhamana katika kutoa maamuzi mbalimbali kuzingatia kanuni na sheria za nchi bila upendeleo wowote.

“Hukumu iliyotolewa na Pilato wakati wa utawala wa Warumi chini ya mfalme Kaisar…haina tofauti na baadhi ya hukumu zinazotolewa hivi sasa katika baadhi ya mahakama nchini hivyo ni vyema wanaokutwa na makosa wakatendewa haki”alisema Mkapa.

Kwa mujibu wa Mkapa alisema mateso ya Bwana Yesu Kristo yaliyopelekea kifo chake yawe fundisho kwa watanzania ambapo wanapaswa kuishi kwa amani na upendo kama inavyompendeza mungu.

Katika ibada hiyo ya ijumaa kuu waumini wa kanisa katoliki parokia ya Masasi walipata fursa pia ya kubusu msalaba ikiwa ni kielelezo,mfano na taswira ya kufundisha kwa lengo la  kujua kwa urahisi jinsi ile mkombozi wao alivyotundikwa juu ya mti ule wa msalaba. 

Aidha ibada hiyo ilihudhuriwa na Rais mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin Mkapa ambaye yuko mjini Masasi kwa mapumziko ya sikukuu ya ufufuko wa bwana yesu Kristo (Pasaka).

TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top