Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

JIMOWACO MKURANGA YADHAMIRIA KUTOKOMEZA MALARIA NA UKIMWI KWA KUTOA ELIMU KWA WANANCHI

TANGAZO

Na Boppe Kyungu,Mkuranga.
Mratibu wa taasisi isiyo ya kiserikali ya  jipeni Moyo Wanawake Community Organisation (JIMOWACO) Israel Musyangi amewataka wananchi wa wilaya ya  Mkuranga mkoani Pwani kuwa na utamaduni wa kupima afya zao mara kwa mara kwa lengo la kubaini afya zao.

Aliyasema hayo jana wilayani humo wakati wa kampeni ya uhamasishaji na upimaji wa virusi vya Ukimwi na Malaria kwa wananchi wa kata za Bupu na Mwarusembe ambapo alisema uhamasishaji huo ulianza Julai 2015 na unatarajia kukamilika Julai 2016.

Alisema hadi sasa zoezi hilo la uhamasishaji limefanyika  katika kata 20 za wilaya ya Mkuranga na kwamba kwa sasa wanatarajia kukamilisha katika kata tano zilizobaki baada ya kupata fedha kutoka kwa wafadhili wa mradi huo.

Alisema katika kata ya Mwarusembe waliojitokeza kupima Malaria ni 50 ambapo kati yao waliogundulika kuwa na malaria ni 11 ambapo kwa upande wa kata ya Bupu wilayani humo waliojitojeza kupima malaria ni 50 huku waliokutwa na virusi vya ugonjwa huo ni 16 pekee.

“Kauli mbiu  ya zoezi hili ni Si Kila homa ni Malaria… ambapo ili kubaini unaumwa nini ni vyema sasa wananchi muwe na utamaduni wa kupima afya badala ya kufanya vitu kwa mazoea au kunywa dawa za malaria bila hata kupima” alisema Musyangi.

Aidha kwa upande wa upimaji wa Virusi vya Ukimwi kwa  kata ya Mwarusembe waliojitokea kupima ni wananchi 48 ambapo waliogundulika kuwa na maambukizi ya  Virusi vya Ukimwi ni wawili na kwa Kata ya Bupu waliopima ni 29 kati yao  wanawake ni 13 na wanaume 19 na kwamba hakuna mtu aliyekutwa na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Kwa mujibu wa Mratibu huyo  alisema mradi wa Tanzania Communication Development Center ulianza  mwaka 2015  na kwamba kwa sasa kinachofanyika ni muendelezo wa mradi huo huku kukiwa na ongezeko la upimaji wa Virusi vya Ukimwi ,afya ya mama na mtoto, pamoja na kifua kikuu.

Issa Athumani (17) mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Mamdi kongo kata ya Bupu ambaye baada ya vipimo alikutwa na malaria alisema katika kipindi cha miezi mitano iliyopita alikuwa anapata maumivu makali  ya kichwa huku akishindwa kutambua tatizo hadi alipopima wakati wa kampeni hiyo na kugundulika na tatizo la Malaria.

Kwa upande wake muelimishaji jamii wa kata ya Mwarusembe Mohammed Kisilwa alisema ni vyema wananchi kila wanapohisi kuwa na  dalili za ugonjwa wa Malaria ni vyema wakaenda hospitali  kwa lengo la kujua matatizo mbalimbali yanayowakabili kwenye miili yao.

Jipeni Moyo Wanawake Community Organisation (JIMOWACO) ni taasisi isiyo ya kiserikali iliyoanzishwa  mwaka 2002, yenye makao makuu yake Kisarawe Mkoani Pwani, ikiwa na lengo la kusaidia akinamama hususani wenye  maambukizi ya Virusi vya Ukimwi waweze kujikwamua kiuchumi.


TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top