TANGAZO
Na Clarence Chilumba, Masasi TC.
Halmashauri ya mji wa Masasi inawahudumia wananchi wake kwa
kuwapatia huduma ya maji safi na salama kupitia mtandao wake wa maji ambao kwa
kiasi kikubwa umefika kila eneo la Halmashauri hiyo.
Mji wa Masasi ni mji ambao unawahudumiwa na vyanzo vya maji vya
aina tatu ambavyo ni Mtiririko, Visima Virefu na Visima Vifupi.
Kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012 Halmashauri ya
mji wa Masasi ina wakazi 102,696 ambapo kati yao wanaopata huduma ya maji safi
na salama ni watu 83,128 ambayo ni sawa
na asilimia 81 ya wakazi wote wa mji huo.
Katika kuboresha upatikanaji wa huduma bora za maji, Halmashauri
ya mji wa Masasi mkoani Mtwara katika mpango wake wa Bajeti ya maendeleo kwa
mwaka wa fedha wa 2015/2016 imepanga kutumia jumla ya shilingi 647,600,000/=
katika idara ya Maji.
Lengo la Halmashauri hiyo ni kuhakikisha upatikanaji wa huduma
bora ya maji safi na salama kwa wananchi wa vijiji vipatavyo 30 kwa asilimia
85.
Kupitia kiasi hicho cha fedha kilichopangwa kitumike Halmashauri
ya Mji wa Masasi imakusudia kufanya mambo yafuatayo ili kuendana na mpango wa
matokeo makubwa sasa maarufu (BRN) ikiwemo uchimbaji wa visima na uwekaji wa
pampu katika vijiji vitano vya Chipole,Mpekeso,Magumuchila,Machenje na
Mlundelunde.
Aidha Halmashauri hiyo kupitia mpango wa Bajeti hiyo imepanga
kufanya ukarabati wa visima vitano vya maji katika vijiji vya Mkapunda, Mumbaka,
Tukaewote, Mkarakate pamoja na Sululu ambapo pia imepanga kubadilisha mfumo wa
genereta kuwa mfumo wa umeme jua katika kisima kilichoko Namkungwi.
Mipango mingine iliyopo ni ile ya kuwezesha ufungaji wa umeme jua
kwa ajili ya usambazaji wa maji safi na salama kwa vijiji jirani kwa mabwawa ya
Machombe na Namikunda pamoja na usimamizi na ufuatiliaji wa miradi hadi ifikapo
juni 2016.
Aidha Mji wa Masasi unapata huduma zake za Maji kutoka kwa Mamlaka
ya Maji Safi na Salama Masasi-Nachingwea (MANAWASA) mradi wenye lengo la
kuwapatia wakazi wa mji wa Masasi huduma bora ya Maji safi na Salama.
Hii ni wiki ya maji yenye kauli mbiu isemayo “MAJI NA MAENDELEO
ENDELEVU”.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD