TANGAZO
Wanasiasa mkoani Mtwara
wametakiwa kuhamasisha wananchi kuona umuhimu wa kuwapeleka watoto
wao shule ili waweze kupata elimu ambayo itawasaidia katika maisha yao ya
baadae kwa kupata ajira kwa kuizngatia kuwa
kwa sasa mkoa wa Mtwara kuna uwekezaji mkubwa
wa viwanda mbalimbali.
Aidha wanasiasa wameaswa kutambua kuwa wana jukumu kubwa la kuwahamasisha wananchi
kupeleka watoto wao shule waweze kunufaika na matunda ya gesi kwa kupata ajira
kwenye viwanda vitakavyojengwa mkoani humo.
Wito huo umetolewa
mwishoni mwa wiki na Katibu Mtendaji wa Shirika la Faidika wote Pamoja la
mkoani Mtwara( Fawopa-Tanzania), Baltazar Komba, wakati natoa misaada
mbalimbali ya vifaa vya shule kwa
wanafunzi wanaoishi katika mazingira magumu kutoka shule mbalimbali za
sekondari mkoani Mtwara.
Alisema wanasiasa
wanapaswa kushiriki ipasavyo katika mapambano
ya kuhamasisha wananchi kupeleka watoto
wao shule kama kwa kuwa wananchi walio
wengi hutegemea sana sauti ya wanasiasa pindi wanapohitaji kufanya maamuzi.
Kwa mujibu wa Komba alisema Wabunge pamoja na madiwani wanapaswa
kuliongelea suala la elimu na kwamba ikiwezekana
watunge sheria ndogo kuhusiana na masuala mazima yanayosababisha watoto wengi kutoripoti shuleni.
“Tatizo kwa sasa hatusikii
sauti zozote za kukemea tatizo hili kutoka kwa wabunge au madiwani kama
wanavyofanya Wakuu wa mikoa na Wakuu wa wilaya kuhamasisha wananchi kuwapeleka
watoto wao shuleni”.alisema Komba.
Hata hivyo Komba,
aliwalalamikia wazazi ambao watoto wao wanaishi katika mazingira magumu ambao
wanasomeshwa na Shirika la Fawopa-Tanzania wanashindwa kufika ofisi za shirika
hilo na kuwaunga mkono kwa juhudi zao za wanazofanya za kuwasomesha watoto wao.
Alisema wazazi waunge mkono jitihada za Fawopa
kwa kuhakikisha watoto wao wanaenda
shuleni kwa kufuatilia mwenendo wao
ikiwa ni pamoja na kukagua mahudhurio yao shuleni na ushiriki wa mtoto katika tendo zima la kujifunza.
Msaada waliopatiwa watoto
hao ni pamoja na sare za shule,viatu, peni, penseli, madaftari makubwa pamoja
na mabegi ya shule kwa ajili ya kubebea
madaftari yao.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD