TANGAZO
Na
Clarence Chilumba, Masasi.
Wakazi wawili wa
kijiji cha Mkalapa Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara ambao ni mume
na mke Said Ngwambo (21) na Rehema Bakari (20) juzi wamehukumiwa kifungo cha
miezi sita kila mmoja kwa kosa la kuharibu kwa makusudi kichanga huku wakijua
ni kosa la jinai.
Mbele ya Jaji wa
mahakama kuu kanda ya Mtwara Dkt.Faudhi Twalibu mwendesha mashtaka wakili wa
serikali Nunu Mangu alidai washtakiwa hao walitenda kosa hilo julai 19, 2013
majira ya saa4:30 huko katika kijiji cha Mkalapa kilichoko Halmashauri ya
wilaya ya Masasi mkoani Mtwara.
Alidai kuwa
washtakiwa hao kwa pamoja waliharibu kichanga kilichokadiriwa kuwa na miezi
minane ambacho kilizaliwa kikiwa hai na baadaye kwenda kukifukia kwenye shimo
jirani na nyumba yao baada ya mume ambaye ni Said Ngwambo kukana kuwa hausiki
na ujauzito huo.
Mangu alieleza kwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo
umekamilika washtakiwa hao wana kosa kosa la kujibu na kuiomba mahakama iwatie
hatiani kwa kuwapa adhabu kali ili iwe
fundisho kwa watu wengine wanaotenda vitendo hivyo vya kikatili kwa watoto.
Washtakiwa hao kwa
pamoja walikubali kuwa walitenda kosa hilo na kuiomba mahakama iwapunguzie
adhabu.
Kwa upande wa utetezi
wa washtakiwa hao ukiongozwa na mawakili Sifael Kulanga pamoja na Robert
Dadaya waliiomba mahakama iwapunguzie adhabu wateja wao kwa kuwa washtakiwa hao
ni mara yao ya kwanza kutenda
makosa na pia mshtakiwa namba moja
Rehema alikuwa na miaka 18 wakati anatenda kosa hilo.
Aidha sababu zingine
zilizotolewa na upande wa utetezi ni kuwa washtakiwa hao wamekaa magereza kwa
muda wa miaka miwili hivyo tayari watakuwa wamepata fundisho kubwa huku
mshtakiwa namba mbili ambaye ni Ngwambo hakuwa na historia ya kutenda makosa
hapo mwanzo.
Baada ya kusikiliza
maelezo ya pande zote mbili Jaji wa
mahakama kuu kanda ya Mtwara Dkt.Faudhi Twalibu aliridhika na maelezo yaliyotolewa na upande
wa mashtaka na kuwatia hatiani
washtakiwa hao kwa kuwapa adhabu ya kifungo cha miezi sita jela kila mmoja .
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD