TANGAZO
Na Fatuma Maumba Wa Mnyeto,Mtwara.
MKUU wa mkoa wa Mtwara, Halima
Dendego, amewataka watumishi wa Serikali kuacha mara moja tabia ya kufanyakazi
kwa mazoea na badala yake waonyeshe uchapakazi wa kweli ili nchi iweze kupata
maendeleo.
Dendego ametoa wito huo juzi wakati
akifungua kikao cha pili cha Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Mtwara kwa mwaka wa
fedha 2014/2015, huku akiwataka watendaji hao kuamka na kufanyakazi
kwa ufanisi bila kusimamiwa na kila mtu acheze kwenye nafasi yake.
“Mimi nasema kipenga kimelia sasa
kila mtu aamke akacheze kwenye nafasi yake tukafanye kazi kama wewe mwandisi wa
barabara basi tuhakikishie wenzio kwamba pale barabara zinapitika ndio tutasema
umefanyakazi sio maelezo au visingizio, kama ambavyo tutamuona muhandisi
wa maji sisi mafanikio ya yeye kuwepo hapa kuona maji yanatoka au meneja wa
tenesco kuona umeme unawaka habari ya kupeana hadithi kwa kweli zimekwisha na
wakati.
“Sasa mimi nawakumbusha katika kikao
hichi tujione hapa Mtwara ni kwetu na sasa hivi ndio kwetu tumekuja hapa kwa
ajili ya kazi tuwafanyie kazi wana Mtwara tuache kufanyazi kwa mazoea…Pia
niwaombe sana Wakuu wa wilaya, Wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri barabara
ndio uchumi na ndio maendeleo makubwa katika nchi yetu hapa msisitizo zile kazi
ambazo mnazitoa naomba mkawe matomaso kwa kuwasimamia wakandarasi wetu tuwaone
wanafanyakazi yenye tija sio kazi ya siku moja tu halafu siku inayofuata
barabara haifai utafikiri haijatengenezwa leo.
Hata hivyo Dendego amewaomba viongozi
hao waelekeze macho yao katika kuhakikisha kwamba barabara za ndani,
Mkoa na za Taifa wanazilinda na kuzitunza kwa kuzifatilia na swala kubwa ni
kuona barabara hizo zinatengenezwa katika kiwango cha ubora wa hali ya juu
kulingana na makubaliano ya kwenye mkataba waliowekeana.
Mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Omari Dendego akizungumza wakati anafungua kikao cha pili cha bodi ya Barabara kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD