TANGAZO
Na Clarence Chilumba, Masasi.
Viongozi wa kimila maarufu Mamwenye wa
wilaya ya Masasi mkoani Mtwara wameelezea kusikitishwa kwao na uamuzi wa Rais
Jakaya Kikwete wa kumwamisha aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Masasi Farida
Mgomi na kumpeleka wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma.
Pia walishindwa kuficha hisia zao
baada ya kueleza kuwa mkuu huyo wa wilaya anayeondoka ndie aliyefanikisha kwa
wao kutambuliwa na viongozi wa serikali na chama kwa ujumla tofauti na hapo
awali ambapo walidharauliwa na hawakupewa thamani yoyote kwa kigezo kuwa wazee
hawana jipya.
Akizumgumza jana kwa niaba ya wazee
hao wa kimila, wakati wa hafla fupi ya makabidhiano na mkuu mpya wa wilaya ya
Masasi katibu wa viongozi hao wa kimila wilaya ya Masasi Mwenye Nakaruma Mchopa
alisema kamwe hawatamsahau mkuu huyo wa wilaya anayeondoka kwa kuwa alikuwa
karibu sana na viongozi hao na aliwapa nafasi ya kutoa ushauri kwa serikali ya
wilaya ya Masasi.
Alisema wakati anateuliwa kuwa mkuu wa
wilaya ya Masasi alikuta wilaya hiyo ikiwa na changamoto nyingi kama vile
tatizo la njaa,maji,mimba za utotoni pamoja na ukiukwaji wa maadili kwa vijana
changamoto ambazo amekiri kuwa kwa sasa zimebaki kuwa historia kwa wilaya hiyo
kutokana na umoja na mshikamano kati ya serikali na viongozi wa kimila.
“Sisi Mamwenye tuko hapa Masasi toka
zamani…lakini hatujawahi kushirikiana na serikali ya wilaya kama
tulivyoshirikiana na mkuu huyu wa wilaya anayeondoka,tulinyanyaswa na
kudharauliwa mbaya zaidi hatukuwa na umoja wetu lakini mara baada ya yeye kuja
Masasi aliweza kutuunganisha na tukaunda umoja wa Mamwenye”.alisema Mchopa.
Kwa mujibu wa katibu huyo wa viongozi
wa kimila wilaya ya Masasi alisema wakati wa uongozi wa Farida viongozi hao
aliwapa fursa ya kukutana ana kwa ana na viongozi wa juu wa serikali akiwemo
Rais Jakaya Kikwete alipofanya ziara ya kikazi wilayani Masasi kitu ambacho
hapo awali hakikuwepo.
Alisema viongozi wa kimila wana nafasi
kubwa katika jamii yoyote nchini katika kutoa elimu ya maadili lakini katika
wilaya ya Masasi hawakuwahi kupewa kipaombele na badala yake walionekana kuwa
ni miongoni mwa watu wasioenda na wakati kulikosababisha jamii kuishi kinyume
na maadili ya kitanzania.
“Hatuna cha kukulipa kwa haya yote
uliyotufanyia zaidi ya kukuombea maisha marefu na mafanikio makubwa katika
uongozi wako… tunaamini ipo siku utakuja kuwa mkuu wa mkoa wa Kusini ambao
mchakato wake wewe ndiye uliyeuanzisha”.alisema.
Kwa upande wake mkuu huyo wa wilaya
anayehamia wilaya ya Chamwino mkoani Dodoma aliwashukuru viongozi hao wa kimila
kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi chake chote cha miaka mitatu ya uongozi
akiwa mkuu wa wilaya ya Masasi mazingira yaliyopelekea kuendelea kuaminiwa na
Rais.
Mwisho
Aliyekuwa mkuu wa wilaya ya Masasi Farida Mgomi akipeana mkono na mkuu mpya wa wilaya ya Masasi Bernald Nduta wakati wa hafla fupi ya makabidhiano ya ofisi.
"Mimi naondoka naelekea wilaya ya Chamwino Mkoani Dodoma Lakini naiacha wilaya ya Masasi ikiwa salama lakini hii yote ni kutokana na ushirikiano wangu na kamati ya ulinzi na usalama...nakuomba endeleza mahusiano hayo".Farida Mgomi.
Mkuu mpya wa wilaya ya Masasi Bernald Nduta akitoa neno la shukrani kwa mkuu wa wilaya anyeondoka Farida Mgomi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD