TANGAZO
Mfuko
wa maendeleo ya jamii TASAF Halmashauri ya mji wa Masasi Mkoani
Mtwara umetoa vifaa vitakavyotumika
katika zoezi la uzoaji wa taka ngumu kwa vikundi viwili vya wanawake wajane
kutoka kata ya Nyasa pamoja na kata ya Napupa Halmashauri ya mji wa Masasi.
Vikundi
vilivyopatiwa vifaa hivyo ni pamoja na kikundi cha Silabu kutoka kata ya Napupa
pamoja na kikundi cha Nyasa B kutoka kata ya Nyasa.
Vifaa
vilivyotolewa na kukabidhiwa kwa vikundi hivyo ni pamoja na magari madogo
mawili aina ya ISUZU
CARRY na vifaa vingine vitakavyorahisisha zoezi hilo lenye lengo la
kuufanya mji wa Masasi kuwa safi pamoja na kuwapatia kipato akinamama hao kwa
kutoza ushuru kwa maeneo watakayozoa taka hizo.
Aidha
kikundi kimoja cha wanawake wajane cha Magumuchila kutoka katika kata ya Mtandi
kimepatiwa vitendea kazi mbalimbali vya ufugaji wa nyuki ikiwemo mizinga kwa
lengo la kutekeleza programu maalumu ya ufugaji nyuki.
Akizungumza
wakati wa hafla fupi ya kukabidhi magari hayo kwa vikundi hivyo
mratibu wa Tasaf Halmashauri ya mji wa Masasi Joram
Msyangi alisema lengo la Tasaf ni kuona kuwa vikundi hivyo vinafikia
malengo yaliyokusudiwa katika utekelezaji wa mradi waliouchagua wa uzoaji wa
taka kwenye maeneo yao.
Alisema kupatikana kwa magari hayo ni ukombozi
kwa wajane hao ambao wamekuwa wakiishi katika mazingira magumu na kwamba
kupitia programu hiyo itawasaidia kuongeza kipato chao kutokana na mradi huo.
Msyangi alisema vikundi hivyo vya wajane vina wajibu
wa kutekeleza mradi wa uzoaji wa taka ngumu pamoja na ule wa ufugaji wa nyuki
kwa mujibu wa taratibu na sheria zilizowekwa na Tasaf na kwamba wawe mfano wa
kuigwa kwenye jamii inayowazunguka.
Kwa
mujibu wa mratibu huyo alisema Halmashauri ya mji wa Masasi imekuwa ikitekeleza
miradi ya Tasaf kwa kiwango cha hali ya juu na kwamba wanatarajia kufikia
malengo yaliyowekwa na serikali ya kuhakikisha kuwa kila mtanzania anakuwa na
maisha bora kupitia miradi ya wanawake na vijana.
Kwa
upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi Andrew
Mtumusha ambaye ni diwani wa kata ya Nyasa aliishukuru Tasaf kwa kutoa
magari hayo kwa wananchi wa kata ya Nyasa huku akiwaasa wanufaika hao kufuata
taratibu za uendeshaji wa miradi hiyo kwa kufuata maelekezo waliyopewa wakati
wa mafunzo.
Mwisho.
MKURUGENZI wa Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Kagoro akiwa na mwenyekiti wa Halmashauri hiyo Andrew Mtumusha wakati wa Hafla ya kukabidhi magari hayo.
Moja ya Gari aina ya ISUZU CARRY lenye namba za usajili T753DDF lililokabidhiwa kwa wanawake wajane wa kata ya Nyasa.
Mratibu wa TASAF Halmashauri ya mji wa Masasi JORAM MSYANGI akiwa na mkurugenzi wa Halmashauri ya mji,mwenyekiti,Mhasibu wa TASAF,Mtaalamu Mshauri pamoja na Ofisa Afya wa Halmashauri ya mji wa Masasi Benjamini Eliasi.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Kagoro akisalimiana na Mtaalamu mshauri wa TASAF.
MTAALAMU Mshauri wa TASAF akimkabidhi funguo za magari hayo mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Kagoro.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Kagoro akimkabidhi funguo za magari hayo mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi Andrew Mtumusha.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi akiwa ndani ya gari hiyo tayari kukabidhi kwa vikundi vya wanawake wajane wa kata ya Nyasa na Napupa
Mtumusha akiongea na wanawake wajane kabla ya kuwakabidhi rasmi funguo za magari hayo.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji akiongea na wanavikundi hao.Hawapo pichani.
Mkurugenzi akitoa neno la shukrani kwa TASAF
BAADHI ya vifaa vya usafi vilivyotolewa na TASAF kwa vikundi viwili vya wanawake wajane wa kata za Napupa na Nyasa B.
MRATIBU wa TASAF Joram Msyangi wakati anatoa maelezo ya mradi huo wa uzoaji wa taka ngumu kwa vikundi viwili vya wanawake wajane.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi Andrew Mtumusha akimkabidhi funguo za gari mmoja wa wanawake wajane.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD