TANGAZO
Na Clarence
Chilumba, Masasi.
Diwani wa kata
ya Sululu (CCM) Halmashauri ya mji wa Masasi Zuberi Mrope (44) amefariki dunia
jana majira ya saa 10:30 usiku katika hospitali ya Mkomaindo Masasi alikolazwa
kutokana na maradhi ya kansa.
Afya ya marehemu Mrope
ilianza kuzorota tangu januari mwaka huu kutokana na kusumbuliwa na maradhi
hayo mazingira yaliyopelekea kushindwa kuhudhuria baadhi ya vikao vya kamati
pamoja na vile vya baraza la madiwani.
Akitoa salamu za
baraza la madiwani mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Masasi Andrew Mtumusha
alisema baraza la madiwani limepoteza mtu muhimu kwenye Halmashauri hiyo pamoja
na Chama cha mapinduzi hasa katika kipindi hiki muhimu cha kuelekea kwenye
uchaguzi mkuu mwezi oktoba.
Alisema marehemu
wakati wa uhai wake alikuwa na uwezo wa kujenga hoja yenye nguvu na si hoja ya nguvu na kwamba alikuwa
mwadilifu kwa wananchi wake waliomchagua kwa kutekeleza ilani ya CCM kuhusu
miradi mbalimbali iliyokuwa inatekelezwa ndani ya kata yake.
Mtumusha alisema
Halmashauri ya mji wa Masasi, baraza la madiwani pamoja na wafanyakazi wote wa
Halmashauri hiyo wanatoa pole kwa familia ya marehemu na kwamba wawe
wastahimilivu hasa katika kipindi hiki kigumu cha msiba.
Alisema marehemu katika kipindi chote
cha uhai wake aliwahi kushika nyadhifa mbalimbali ndani ya chama na serikali
ikiwemo mwenyekiti wa iliyokuwa mamlaka ya mji mdogo wa masasi, mwenyekiti wa
kitongoji cha ghalani huko Sululu, mwenyekiti wa kamati ya maadili ya baraza la
madiwani 2014/2015 na kwamba hadi kifo chake alikuwa ni diwani wa kata ya Sululu
Halmashauri mji wa Masasi.
Kwa upande wake mjumbe wa Halmashauri
kuu ya Taifa CCM (MNEC) wa Wilaya ya Masasi Ramadhani Pole alisema Chama Cha
Mapinduzi kimepoteza diwani wake ambaye ni mmoja wa wanachama waadilifu wa
chama hicho na kwamba ameacha pengo kubwa kwa Chama.
Alisema marehemu amewahi kushika
nyadhifa mbalimbali za uongozi ndani ya Chama ikiwemo mjumbe wa mkutano mkuu wa
kata,mjumbe wa Halmashauri kuu ya kata ya Sululu,Mjumbe wa Halmashauri kuu
wilaya pamoja na mjumbe wa mkutano mkuu wa mkoa wa Mtwara na kwamba kwa
kuthamini mchango wake walitoa rambirambi ya shilingi 500,000.
Marehemu Mrope alizaliwa julai 3, 1971
katika kijiji cha Sululu kilichoko kata ya Sululu Halmashauri ya mji wa Masasi na alipata elimu ya msingi katika shule ya
msingi Sululu kati ya mwaka 1981-1987 na ameacha mjane na watoto sita.
Mwisho.
Mamia ya waombolezaji wakiwa kwenye ibada ya mazishi nyumbani kwa marehemu Zuberi Peter Mrope (MANDOZA) aliyekuwa diwani wa kata ya Sululu.
PADRE wa Mtaa wa Sululu wa kanisa la Anglikana jimbo la Masasi akiwaongoza waombolezaji waliojitokeza kumuaga kipenzi wao,diwani wao wa kata ya Sululu Halmashauri ya Mji wa Masasi.
GARI lililobeba jeneza lililokuwa na MWILI wa marehemu ZUBERI PETER MROPE aliyekuwa Diwani wa Kata Ya Sululu likielekea eneo la Makaburi Kijiji Cha Sululu.
Wakazi wa Sululu na maeneo jirani wakiwa wamebeba jeneza la marehemu MANDOZA
MKE wa Marehemu wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Sululu Zuberi Peter Mrope akisaidiwa na majirani kutoka kwenye eneo la makaburi mara baada ya mazishi ya mume wake.
Wananchi wakifukia kaburi la Marehemu Peter Zuberi Mrope aliyekuwa diwani wa kata ya Sululu.
Wananchi wa kijiji cha Sululu na maeneo jirani waliokuja kumsindikiza katika safari yake ya mwisho marehemu ZUBERI PETER MROPE wakimsikiliza mbunge wa jimbo la LULINDI Jerome Bwanausi wakati anatoa salamu za serikali kwa familia ya marehemu.
MWENYEKITI wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Andrew Mtumusha akitoa salamu za rambirambi kwa familia na wakazi wa kata ya Sululu kwa kuondokewa na diwani wao.
Mamia ya waombolezaji waliojitokeza kwenye mazishi ya Diwani wa kata ya sululu Zuberi Peter Mrope (MANDOZA)
KATIBU Msaidizi wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Masasi AJALI MPATAGA akitoa salamu za CCM kwa familia na wakazi wa kata ya SULULU kwa kifo cha marehemu Diwani wa kata hiyo Zuberi Peter Mrope ambapo Chama Cha Mapinduzi wametoa rambirambi ya fedha kiasi cha shilingi 570,000/= kwa familia ya marehemu.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD